Mtoto amebadilisha Channel

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,430
Jana nimeenda kwa jamaa yangu kumtembelea baada ya kutoanana nae kwa muda kidogo.

Wakati nipo hapo nyumbani kwake tukawa tunatazama Tv mechi ya Simba na Biashara.

Katikati ya mechi mwenyeji wangu akatoka nje kuongea na simu, pale ndani tukabaki mimi mtoto wa miaka kama mitano hivi, basi muda huo huo akachukua remote na kuweka channel cartoon, na dogo hasemezeki, baba mtu alivyorudi nae akawa anaangalia Cartoon tuu.

Basi mpaka naaga sikua na matokeo kamili ya mechi.
 
Nani sasa ambaye ni mjinga hapa kati ya baba na mtoto?
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hapo aliyezingua ni Baba, sio mtoto.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Hahaaa huyo baba ina maana hana kauli kwa mtoto wake? Hata ile ya pls Junior na bla bla kibao alikosa!!

Anyway simba tulishinda 4-0, huku Chelsea tukilala 2-0..
Bora tumeshinda, matokeo mengine yeyote ingekua balaa
 
Hahaaa huyo baba ina maana hana kauli kwa mtoto wake? Hata ile ya pls Junior na bla bla kibao alikosa!!

Anyway simba tulishinda 4-0, huku Chelsea tukilala 2-0..
Nje ya mada

Hiyi avartar yako tu.....
 
1. Inawezekana malezi ndio tatizo
2. Inawezekana baba hakujua nani kabadili
3. Wageni wengine huwa na shida ya kuvuruga ratiba za watu, so mbinu za kimedani kuwatoa hutumika (ukweli mchungu)
4. 1,2 & 3 are correct answers
 
Hayo mambo ndo maana nilinunua TV 2 maana unakuta mm nataka mpira utasikia mke anataka aangalie marudio ya slay Queen, Mara badilisha king'amuzi cha dstv weka azam nataka kuangalia single mama hapana mpira una raha yake ila huyo mtoto ningemfurusha potelea pote! Hahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…