Mtoto ana miezi minne, anna mimba nyingine

Mtoto ana miezi minne, anna mimba nyingine

SUZANE

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
740
Reaction score
500
Heri ya mwaka mpya wapendwa.

Natoa shukrani zangu kwenu nyote mlionishauri na kunifariji wakati nikiwa nahitaji mtoto, hamkuniacha mpweke mpaka mimba ilipotunga na niliwajulisha, sasa Mungu amenipa mtoto mume, na mzuri kwa kweli. Glory to God.

Leo naombeni mnisaidie kuhusu huyu wifi yangu jamani, ndio kwanza mtoto bado mdogo anamimba nyingine ya mwezi mmoja sasa.

Alizaa kwa oparetion,

Mumewe anamwambia azae, wengine atoe, ndio kanifuata nimshauri, binafsi nimemwambia anipe muda.

Mie si mzoefu kabisa wa mambo haya ndio maana ckutaka kukurupuka kumwambia chochote.

Hivi kweli inawezekana oparetion yake kuhimili mimba nyingine??

Kutoa mimba wakati kuna watu wanasaka watoto ka mie itakuaje, kwanza kwa imani yangu ni dhambi kubwa.

Kama kawaida kama hujickii kujibu pita wima, itakua heshima kwako.

Nawasilisha kwenu.
 
Aende hospitali hasa oale alipofanyiwa surgery hiyo wampe ushauri, ndio wanaofaham complication yake. si tatizo sana ila anaihtaji routine clinic attendance, toa HOFU...TUMAINI LIWEKE KWA BWANA...
 
Oooh!! Hilo nalo neno haswaa
 
Kitaalamu haishauriwi nae wakat anahudhuruia clinic baada ya operation nadhan aliambiwa muda wa kukaa kabla ya kuconceive so amekiuka maagizo arud akapewe njia mbadala kule alikofanyiwa operation itakuwa vizur zaid....but hiyo hali haishauriwi na nina uhakika hundred percent nae alijua hilo....poleni Mungu awape wepes
 

Utamu huu jamani sasa yeye anakiachia mapema hivi! But no sweat aone what do after she had seen dokta make anaweza kuitoa au akaiacha ila ajipange kumlisha huyo dogo wa mbele.
 
UKijifungua kwa njia ya upasuaji, unashauriwa kubemba mimba nyingine mpaka baada ya miaka minne. Miezi minne huyo mtoto bado mdogo sana na mama yupo kwenye hatari ya kupata madhara. Mtoto itabidi akatishwe vitu kama maziwa ya mama. Aende hospitali kupata ushauri au matatizo yanamngojea tena makubwa sana.
 
Ukubwa dawa, nawashukuru sn
 
Back
Top Bottom