kama lishe yake ni duni mwanamke mwenye mapungufu ya folic acid mwilini anaweza kuzaa mtoto mwenye matatizo kwenye ubongo na mishipa ya fahamu.
Njia pekee ya kuzuia ni mwanamke kuanza kutumia hizo dawa miezi miwili KABLA ya kupata ujauzito mpaka miezi mitatu ya mwanzo ya mimba.
Kwakua mimba nyingi haziko planned, hua ni za bahati mbaya ni vyema akaanza kutumia hiyo dawa miezi sita au mwaka mmoja kabla ya ujauzito
(Dose ya folic acid ni 0.4mg kwa siku, ila kama mwanamke mtoto wake wa kwanza alizaliwa na matatizo hayo, mimba inayofuata atapewa dose kubwa- 5mg kwa siku)....Subiri mtoto azaliwe kama tatizo lipo atatibiwa na madaktari wa upasuaji.