Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimesikiliza kwa masikio yangu kupitia ITV Dr wa Mwanyamala Hospt akisema hayo leo usiku
Naomba wataalamu mnifafanulie hili
ARV atapewa kama CD4 zake tayari zimeshuka sana mwilini mara baada tu ya kumaliza kubakwa!
Inaitwa PEP yaani Post Exposure Prophylaxis.Ni mchanganyiko wa dawa za ART ambazo hupewa mtu(si lazima awe mtoto tu) katika kipindi kisichozidi saa 72 baada ya kitendo chochote kinachomweka kwenye hatari ya kuambukizwa HIV mf kubakwa ama kunajisiwa,kwa madaktari kujichoma bahati mbaya na sindano ama kitu chenye ncha kali viliyotumika kumhudumia mwathirika ama mgonjwa unayemhudumia.Ukiona mtoto kanajisiwa ama kabakwa muwahishe hospitali ya serikali akapate huduma hiyo upesi ndani ya saa 72.
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Sio mtoto tu...ukibakwa especially kwenye nchi zetu hizi kuna uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa ukimwi ukiwa mmojawapo!
Utaratibu ni kwamba utafanyiwa vipimo vya haraka vya ugonjwa wa zinaa ...kama unao utahitaji tiba na kama hauna utatakiwa kupewa kinga!
Mojawapo ya kinga ni madawa ya ARV ...tunaita PEP(post exposure prophylaxisis) kama alivyosema mdau hapo juu.
nawashukuru sana kwa somo, kama nilivyosema hapo awali njia za kujifunza ni adha kuuliza sana au kujifanya UNABISHA ili uendelee kupata nondoUsiongee kitu usichokijua mkuu utakuwa unapotosha jamii.Si vizuri ingawa unachosema ni kweli kwa mtu aliyebakwa akiwa tayari alikwishaathirika.Huyu hatapewa PEP isipokuwa atatibiwa tu magonjwa mengine kama yapo na kuhusu ARV atatumia wakati muafaka CD4 zitakaposhuka chini.Kwa mtu ambaye hakuwa na HIV halafu akabakwa hupewa hizo ARV kama kinga kama nilivyoeleza hapo juu.
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums