Ulirchdov
JF-Expert Member
- Apr 4, 2019
- 356
- 258
Wakuu habari za wakati? naomba msaada wenu wa kitabibu juu ya tatizo hili linaloniumiza kichwa
Mwanangu wa miezi mitatu (3) anasumbuliwa na meno ya plastiki, mtoto amekuwa akilia sana hasa wakati wa usiku ndipo jana nikaamua kuwa wazi kwa jirani yangu ambae kidogo ana utaalamu na magonjwa ya watoto ila hawezi kutibu, alimfanyia mwanangu uchunguzi wa kawaida akabaini atakuwa anasumbuliwa na meno ya plastiki ambayo amesema huwa yanawasumbua sana watoto wachanga nilipomuuliza chanzo cha tatizo hilo alisema hana uelewa juu ya hilo zaidi ya kusema nimtafutie mwanangu dawa ilinishangaza kidogo iweje mtu aweze kusema ni meno ya plastiki halafu asijue chanzo ni nini au yanatokana na nini, sikutaka kumhoji sana.
Sasa wakuu naomba kuuliza ni nini chanzo cha tatizo hili? na je, mwanangu apatiwe dawa ipi aweze kupona?
Ni imani yangu kwamba Jf imesheheni wataalamu na watu mbalimbali wenye utaalam na upeo wa kitabibu watakaoweza kunipa ushauri na mawazo ya kitaalam ili mwanangu aweze kupona. Naomba msaada wenu wakuu!!