Hivi ninyi mnaopinga ubaba wa jamaa mna nini? Baba alikuzaa viunoni mwake acheni bana. Nimeshuhudia kijana aliyekataliwa na baba yake akiwa mtoto; akakuzwa na mama akishirikiana na baba wa kambo wa kijana (mume wa mamaye). Baadaye yule kijana alipokuwa mkubwa alimuuliza mama yake "baba yake mzazi ni nani." Pamoja na kuambiwa juu ya uovu wa babaye, yule kijana aliamua kufunga safari ya kwenda mbali kumtafuta baba yake mzazi. Alisema "Nataka kumjua baba yangu aliyenizaa hata kama hakunitunza. Namtaka baba". Alifika huko, akamkuta baba yake. Akafurahi sana, roho yake ikatulia. Akasema, "sasa ni mtu, najua nasaba yangu kwani nimemjua baba. Najisikia mwenye thamani. Roho yangu imetulia. Nami ni mtu kati ya watu." Jamani mnaelewa hilo?? Mnaona faida ya baba? Kama ubaba ni kitu kirahisi kwa nini kijana asiridhike na baba wa kambo (mume wa mamaye) aliyemtunza; tena vizuri tu? Mtoto asidhulumiwe baba yake. Mpeni haki yake hata kama baba ni wa ajabu kwani damu ya mtu haipotei.