Mtoto apewe last name gani

Massawe, Mushi, Mboya, Chuwa, KIssima, Lema, Mallya - chagua mojawapo lakini gharama yake ni mbuzi

Hakuna hata moja hapo tena yote hayo na matelekezaji kishenzi, hawasaidii kitu ni kujisifu tu nina mtoto na fulani tena wakiume aisee.
 
nani kama baba tena huyo baba wa vijarida nae wamuhesabu ni sawa na kutaka kulipwa mshahara wa jambo ambalo wengine wanafanyia kazi ushaona wapi
Nani kama baba?!! Haijalishi kama anamtunza au hamtunzi lakini ndo mzazi wake (baba yake). Ndo kamzaa kutoka viunoni mwake. Hiyo mtu hawezi kubadili. Kumbe aitwe jina la baba yake mzazi tu. Hakuna jinsi. Mtu huwezi kujichagulia wa kukuzaa.
 
Mtoto nae anamhitaji baba, akikua atahitaji kujua alipotokea(roots) nafikiri aendelee kutumia jina la babaye! Mahusiano mabovu ya baba na mama yake yasisababishe akakosa haki yake,
 
It doesn't matter the dad is the dad! hivyo last name should be dads! mengine hayo ya socio economic mtayahandle mnavyojua! yasiingilie norms tank youu!
 
yaani ukiangalia kwa undani viumbe wana maudhi hawa saa nyingine.. The last tym waliongpea kwa simu huyo kaka akawa anajishebedua matokeo yake bi dada akamwambia 4get u ever had a child with.. Inakera kwa kweli.

wana maudhi kupita kiasi. Mi sista angu huwa anamwambia u r his biological father but hutaona jina lako kwenye pepaz za mwanangu,na ni kweli mtoto anatumia majina yake matatu shuleni hayana uhusiano na babake. Wanaume wanajua kututenda jamani.
 
kama mtoto ni wangu ningemuita Katarina Perpetua Sarwat Gwandu, Sijui mambo ya John Lema hiyo ni kimpango wake....pambaf.....
 
Huyo mtoto apewe jina la Baba yake tu kwani hata iwaje ipo siku mtoto atakuja kuuliza baba yake sasa cha muhimu ni bora hata kuacha maswali mwengi kwa mtoto atakapo kuwa!
 
Hivi ninyi mnaopinga ubaba wa jamaa mna nini? Baba alikuzaa viunoni mwake acheni bana. Nimeshuhudia kijana aliyekataliwa na baba yake akiwa mtoto; akakuzwa na mama akishirikiana na baba wa kambo wa kijana (mume wa mamaye). Baadaye yule kijana alipokuwa mkubwa alimuuliza mama yake "baba yake mzazi ni nani." Pamoja na kuambiwa juu ya uovu wa babaye, yule kijana aliamua kufunga safari ya kwenda mbali kumtafuta baba yake mzazi. Alisema "Nataka kumjua baba yangu aliyenizaa hata kama hakunitunza. Namtaka baba". Alifika huko, akamkuta baba yake. Akafurahi sana, roho yake ikatulia. Akasema, "sasa ni mtu, najua nasaba yangu kwani nimemjua baba. Najisikia mwenye thamani. Roho yangu imetulia. Nami ni mtu kati ya watu." Jamani mnaelewa hilo?? Mnaona faida ya baba? Kama ubaba ni kitu kirahisi kwa nini kijana asiridhike na baba wa kambo (mume wa mamaye) aliyemtunza; tena vizuri tu? Mtoto asidhulumiwe baba yake. Mpeni haki yake hata kama baba ni wa ajabu kwani damu ya mtu haipotei.
 
Babuyao nawafahamu wawili ambao hawataki hata kuwasikia hao baba zao!Na wanasema kabisa kua wa kambo ndio baba coz yeye ndie alimlea na jina alikua na la baba mzazi ila kabadilisha kwa hiari...sasa anatumia la baba wa kambo!Kila mtu ana uhuru wakuchagua...sasa hivi mtoto hawezi kuchagua kwa hiyo mama amchagulie linalompendeza..akikua atabadilisha akitaka!Alafu kwani akiwa na jina la mama ndo hawezi kuonyeshwa baba yake akitaka??Sioni uhusiano wa jina na kumfahamu baba!
 
Lizzy, jina la baba la maana sana kwa sababu linaonesha nasaba ya mtu; ni sehemu kubwa ya identity yake. Ndo maana kati ya majina ya mtoto kuna sehemu ambapo jina la baba linatajwa. Sasa mama anapotumia kigezo cha mahusiano mabaya kati yake na baba mtoto kumnyima mtoto jina la baba yake nadhani si sawa. Ni afadhali jina hilo liandikwe kwanza ili atakapokua kama atalikataa basi ndo abadilishe mwenyewe.

Nimezungumzia juu ya kijana kwenda kumtafuta baba yake kutaka kuonesha bond iliyopo kati ya mzazi na mwanaye; bond ambayo inapaswa kuoneshwa hata kwenye utambusho wa mtoto katika kutumia jina la baba yake licha ya tabia zake ambazo pengine si nzuri.

Umezungumzia watoto waliokataa majina baba zao kwa vile baba hao hawakuwa na muda nao. Hayo ni matukio ya kusikitisha sana. Lakini ujue kwamba hata hao vijana deep down katika nafsi zao ni watu wenye ombwe na crisis fulani hata kama wanaonekana wana furaha. Watakuwa na simanzi na huzuni ya moyo na roho inayojionesha kwa nje kwa njia ya hasira na hata kukataa majina ya baba zao walio wazaa.
 
kama mtoto ni wangu ningemuita Katarina Perpetua Sarwat Gwandu, Sijui mambo ya John Lema hiyo ni kimpango wake....pambaf.....
hahahaha Preta umenifurahisha pambaf na nusu!
 

babu yao kama unaandika tamthilia vile.. Huyo mtoto mwenyewe ana miaka 6 but yuko tight anajua anahangaikiwa umamani aliwahi kusema "mimi baba yangu hanifai hata anitafuti" mamaye akamkataza kusema hvyo tena but mtu baki unaweza sema amefundishwa.. Watoto wanaona na kujua kila wanalotendewa tena hawa wa dot com ogopa..
 

Sio kama napingana na wewe ila kuna pande mbili kwenye kila kitu....
Ila hapo kwenye bold sikubaliani na wewe hata kidogo....wapo wenye wenye hayo majina na baba zao karibu lakini bado wakawa kwenye hali ya huzuni kwasababu huyo baba hamsaidii chochote wala kumjali.....na tunaowazungumzia wapo wenyewe furaha na amani mioyoni mwao zaidi ya ambavyo wangekua kama wangekua na mahusiano na baba zao!!!Jina halijengi mtu......ila mtu anajijenga mwenyewe kulingana na mazingira!!
 

Tell them Lizzy!
Nimefurahishwa na mitazamo yenu Great thinkers ntafikisha maoni km yalivyo!!
 
Tutofautishe kati ya identity ya mtoto na matunzo ya mtoto. Identity ya mtu likiwemo jina lazima iwe kamili, yenye ukweli na bila ulaghai au kificho. Matunzo ya mtoto yanaweza kufanywa na yeyote yule: mjomba wake, baba wa kambo (mume wa mamaye), babu yake (mzaa mamaye). Lakini matunzo hayo hayawezi kubadili ubini wa mtoto au identity yake. Ndo maana nakataa kutoandika jina la baba yake hata kama ni wa ovyo namna gani kwani ndo identity ya mtoto huyo. Huyo ndo aliyemzaa hata aweje. Identity ya mtoto (nasaba) yaweza kubadilika tu kwa njia ya legal adoption. Kwa njia hii mtoto anakata/katishiwa uhusiano wa awali ambao ulikuwa si legal tu bali pia na hasa natural na kuchukua uhusiano mpya wa adoption. Hapo anaweza kubadilishiwa hata jina baba yake wa kumzaa (natural father) na kuandika jina la legal father.
 
Mtoto kupewa jina la mama yake sidhani kama itakuwa ni ungwana hakika huyo mtoto atakuja kujiuliza maswali mengi sana mbeleni kwani mtoto jina lake mfano anaitwa Pepetua Mariam kesho atakapokuwa akitumia kwa ujumla litamuumiza sana. Mfano toka nianze mimi kusoma sehemu zote nilizopita hata kila ninapopita sijawahi mtu kuuliza jina la Mama yako nani mara uulizwapo jina lako kamili lazima la baba liwepo.
Ni sawa kuwa wapo wanaume wengi sana huwakataa watoto kwa sababu zao binafsi lakini swala la kumpa mtoto jina sioni kama linaweza kulipa machungu ya matunzo kwa mtoto huyo.
 

Kwanini uwe na jina la mtu ambae hataki kua na uhusiano na wewe????Kama hataki kukutambua jina lake litakua vipi lako???
 
Massawe, Mushi, Mboya, Chuwa, KIssima, Lema, Mallya - chagua mojawapo lakini gharama yake ni mbuzi


No! no! no!, bali Mwakasyuka, Mwanginde, Mwanyingili, Mwasandube, Mwakisi, Mwandumbya, Mwandosya, Mwasakafyuka, Mwantepanya etc please.
 
mmmhhhh haya mambo nimeyapitia na mie natumia jina la mwisho la mama yangu....

Si haki, basi mtafute siku wewe na mamii ili mumrudishie mbegu yake mzee wa watu aliyoitoa( biological father) ili muwe free na maisha kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…