Mtoto atakuumbua

Mtoto atakuumbua

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Mke na mume waliobarikiwa kuwa na mtoto mmoja mdogo walipendana sana na daima walitaka kudhihirisha upendo wao kwa watu ikiwa ni pamoja na kushikana mikono, kuitana majina matamu kama "honey, Darl, Dear, Switiiii" nk nk.

Siku zote mmoja wao akiwa anatoka huwa ana muaga mwenzie na mtoto kwa staili ya busu na kukumbatiana. Mtoto alizoea hali ya mapenzi ya wazazi.

Siku moja wapenda nao hao waligombana sana usiku na kurushiana kauli zisizofaa kuhusu mapenzi yao. Mke akakasirika sana, na akiwa anataka kwenda kazini asubuhi, hakutaka hata kumuaga kabisa mumewe ambaye alikaa sebuleni na mtoto kwa staili aliyozoea. akambusu tu mtoto na kufungua mlango kutaka kuondoka ....

Lakini ghafla mtoto akamuuliza: "mamiii...." mama alipogeuka na kuitika, "yes mai dia": mtoto akauliza: ...."Maiii why today you don't want to kiss mai Dadiii...., are u okei??" mtoto akamkimbilia mama na kushika mkono kumrudisha ndani ili ambusu japo kidogo tu "dadiii wake".

Mama akajisikia aibu sana nafsini mwake, akarejea na kumbusu "Dadiii"!japo kwa shingo upande...Dadiii nae pia ikamwingia hiyo!.

Tafadhali usijaribu kuonyesha mabadiliko au yake mapenzi yetu ya kuigiza mbele ya mtoto/watoto.
 
Mke na mume waliobarikiwa kuwa na mtoto mmoja mdogo walipendana sana na daima walitaka kudhihirisha upendo wao kwa watu ikiwa ni pamoja na kushikana mikono, kuitana majina matamu kama "honey, Darl, Dear, Switiiii" nk nk.

Siku zote mmoja wao akiwa anatoka huwa ana muaga mwenzie na mtoto kwa staili ya busu na kukumbatiana. Mtoto alizoea hali ya mapenzi ya wazazi.

Siku moja wapenda nao hao waligombana sana usiku na kurushiana kauli zisizofaa kuhusu mapenzi yao. Mke akakasirika sana, na akiwa anataka kwenda kazini asubuhi, hakutaka hata kumuaga kabisa mumewe ambaye alikaa sebuleni na mtoto kwa staili aliyozoea. akambusu tu mtoto na kufungua mlango kutaka kuondoka ....

Lakini ghafla mtoto akamuuliza: "mamiii...." mama alipogeuka na kuitika, "yes mai dia" mtoto akauliza ...."why today you don't want to kiss mai Dadi...., are u okei??" mtoto akamkimbilia mama na kushika mkono kumrudisha ndani ili ambusu japo kidogo tu "dadiii wake".

Mama akajisikia aibu sana nafsini mwake, akarejea na kumbusu "Dadiii"!japo kwa shingo upande...Dadiii nae pia ikamwingia hiyo!.

Tafadhali usijaribu kuonyesha mabadiliko ya penzi lenu mbele ya mtoto/watoto.
safi sanaa
 
hhahhahahhahahha keep it up mtoto, atakama ni shingo upande lkn ni kisss,
 
Ngoshwe umekumbusha kitu muhimu sana.
Na pia wanandoa msipende kuonyesha chuki kwa watu (mathalani majirani zenu) mbele ya watoto siku uki'pretend kuwapenda, mtoto atakuumbua.
 
Ngoshwe umekumbusha kitu muhimu sana.
Na pia wanandoa msipende kuonyesha chuki kwa watu (mathalani majirani zenu) mbele ya watoto siku uki'pretend kuwapenda, mtoto atakuumbua.

That true...kuna wale wazazi wanaokaa na watoto anawaambia msiende kula kwa mama fulani "mchawi" ..utoto akishika hilo hata akipewa pipi na mama fulani atasema "mama kankataza kula kwa watu, eti we mchawi"...au baba hataki mdeni wake ajue yupo akimwambia mtoto akija mgeni mwambie baba hayupo: Mtoto atai copy hivyo hivyo..."eti baba kaniambia akija mgeni niseme hayupo"..ukiullizwa yupo wapi:, atakuumbua "si amelala na mama mwenyewe huko chumbani kwake!"

yupo mtoto wa kiume alikatazwa na mama yake: " We Jack, usilale huko chumbani kwa dada zako wewe mwanaume!.."

Mtoto akadadisi saaaana, siku alipoenda shule akafundishwa kwa mifano kuwa "baba yake ni Mwanaume kama yeye na mama yake ni mwanamke kama dada zake. Aliporejea nyumbani akamuuliza mama yake, "eti mama we ulisema mimi nisilale kwa kina dada,.. mbona baba analala chumbani kwako??, mama akakosa jibu lenye mantiki akaishia kumwambia "babaako mkubwa!" (you can guess the next question..)
 
huyo mtoto engekuwa wangu sana mtoto hata kama wamekiss kwa unafiki,ila ukweli watoto huwa wanaunganisha familia
 
Back
Top Bottom