jobel
JF-Expert Member
- Mar 26, 2013
- 321
- 174
Wanajamvi, poleni kwa majukumu.Kuna mtoto wa kiume wa shemeji yangu mwenye umri wa miaka minne na ushei,ana tabia ya kunusa nepi iliyotumika(yaani si mpya) ili aweze kupata usingizi.
Usiku anapopanda kitandani ni lazima pawepo na nepi ambayo huichukua na kuanza kuinusa hadi usingizi unamchukua, na analala ameishikilia mkononi.
Amefanya mama yake anapokwenda kutembelea nduguze aombe nepi zilizokwisha tumika ili ampelekee mwanae.
Na kila anapopewa anafurahi kupita kiasi kana kwamba amepewa kitu cha thamani kubwa sana.
Naomba kwa wataalamu wa tabia za watoto na yeyote mwenye ufahamu wa hiyo tabia ya huyo mtoto anijuze kama anakabiliwa labda na upungufu wa madini fulani mwilini na nini afanyiwe ili kuachana na tabia hiyo ya kunusa nepi zilizokwisha kutumika.Asanteni.