Mtoto hapati usingizi mpaka anuse nepi iliyotumika kwanza

Mtoto hapati usingizi mpaka anuse nepi iliyotumika kwanza

jobel

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
321
Reaction score
174
Wanajamvi, poleni kwa majukumu.Kuna mtoto wa kiume wa shemeji yangu mwenye umri wa miaka minne na ushei,ana tabia ya kunusa nepi iliyotumika(yaani si mpya) ili aweze kupata usingizi.

Usiku anapopanda kitandani ni lazima pawepo na nepi ambayo huichukua na kuanza kuinusa hadi usingizi unamchukua, na analala ameishikilia mkononi.

Amefanya mama yake anapokwenda kutembelea nduguze aombe nepi zilizokwisha tumika ili ampelekee mwanae.

Na kila anapopewa anafurahi kupita kiasi kana kwamba amepewa kitu cha thamani kubwa sana.

Naomba kwa wataalamu wa tabia za watoto na yeyote mwenye ufahamu wa hiyo tabia ya huyo mtoto anijuze kama anakabiliwa labda na upungufu wa madini fulani mwilini na nini afanyiwe ili kuachana na tabia hiyo ya kunusa nepi zilizokwisha kutumika.Asanteni.
 
Mazoea hujenga tabia. Mbona kwa umri alio nao sidhani kama kulala mpaka kibembelezeo. Wameshamzowesha huyo. Ila wana kazi ya ziada ili waweze kumbadilisha.
 
Hapo hakuna cha upungufu wowote mwilini,mtoto huzaliwa hajui chochote hivyo hujaribu kila kitu hata hujaribu kushika hata moto.Huyu hukuzuiwa kunusa kitu hiyo hivyo akafanya mazoea dawa ni kumzuia tu,aking`ang`ania asimnyime mapiga huo ujinga utamtoka mtoto kwa kiboko.Mtoto umleavyo ndiyo akuavyo,.......mkunje samaki angali mbichi. au hujaona watoto wengine wananyonya vidole hata wakubwa,wengine wanajinyea ili hali ni wakubwa kabisa...tatizo malezi.
 
Duh! Kweli dunian kuna mambo! Anaulea huo ugonjwa utakuwa mkubwa.
 
Akikua anaacha, walimzoea alivyokuwa mdogo.
Wengine hulilia kanga aiweke karibu na mdomo, wengine kitambaa kama leso anakishika shika. Ni njia tu ya kujibembeleza aliyozoea.
 
Hilo tatizo la mtoto ni la kiroho. Ana jini linakompa kupenda harufu ya nepi iliyotumika, akiinusa huwa linapata nguvu au mlango wa kuingia na kumchukua na kumpeleka kutumikishwa. Baada ya miaka kadha aweza kuwa zezeta, kichaa n.k. Dawa ni maombi na pepo hilo litamwacha.
 
Hapo hakuna cha upungufu wowote mwilini,mtoto huzaliwa hajui chochote hivyo hujaribu kila kitu hata hujaribu kushika hata moto.Huyu hukuzuiwa kunusa kitu hiyo hivyo akafanya mazoea dawa ni kumzuia tu,aking`ang`ania asimnyime mapiga huo ujinga utamtoka mtoto kwa kiboko.Mtoto umleavyo ndiyo akuavyo,.......mkunje samaki angali mbichi. au hujaona watoto wengine wananyonya vidole hata wakubwa,wengine wanajinyea ili hali ni wakubwa kabisa...tatizo malezi.

Asante kwa ushauri mkuu.
 
Akikua anaacha, walimzoea alivyokuwa mdogo.
Wengine hulilia kanga aiweke karibu na mdomo, wengine kitambaa kama leso anakishika shika. Ni njia tu ya kujibembeleza aliyozoea.

Mkuu Kongosho, asante kwa ushauri.
 
Hilo tatizo la mtoto ni la kiroho. Ana jini linakompa kupenda harufu ya nepi iliyotumika, akiinusa huwa linapata nguvu au mlango wa kuingia na kumchukua na kumpeleka kutumikishwa. Baada ya miaka kadha aweza kuwa zezeta, kichaa n.k. Dawa ni maombi na pepo hilo litamwacha.

Mkuu Victor Kapande, asante kwa ushauri mzuri ubarikiwe.
 
OK mkuu,nakushukuru pia kwani ni mtazamo wako.
 
badala ya kumpa nepi,angepewa kitu kingine cha kumsaidia alale nacho,kama ki gari kidogo,au kama wa kike mdoli.hayo ni mazoea tu kwa kuwa mama anamuachia na yeye anaendelea nayo.watoto wakikua wanakuwa na stage zao za vituko vyao,mwisho wa siku ataacha.ila la kunusa nepi nahisi sio mazoea mazuri
 
Hadisi njoo!
Uwongo njoo!
Ushankolea!
...
Afu ata haichekeshi!
 
huyo mtoto anatumia nepi kama kitu cha kucuddle nacho,atafutiwe teddy bear au cuddle cloth awe analala nayo mfano kama hii

images.jpg
images1.jpg
images2.jpg
 
Attachments

  • 12371_Teddykompaniet_Teddykompaniet__koseklut_kani_1.jpg
    12371_Teddykompaniet_Teddykompaniet__koseklut_kani_1.jpg
    16.9 KB · Views: 69
Nashauri apelekwe kwenye maombi pia jaribu kukaa karibu na mama mwenye mtoto muulize kama hajajihusisha na miujiza ya giza kupata huyo mtoto. Tabia ya kuwashirikisha waganga ili upate mtoto huibua sintofahamu nyingi yapaswa zipigwe vita na tumkabidhi Mungu shida zetu yeye ndiyo jibu.
 
Aligunduaje ?..., I mean ilikuwaje hadi akajua nepi itamlaza , what happen kwa mara ya kwanza ?
 
Back
Top Bottom