Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Wapendwa naombeni mnisaidie katika hili, huyu mtoto ashanichosha ana miezi minne tu ila hataki kabisa kunyonya, alianza kama miezi miwili hivi ikabidi wa tatu nianze kumpa maziwa ya fomula ila sasa naona kawa too much siku nzima hajaonja hata tone yupo bize ananyonya kidole tu...hapa namuona ana njaa kabisa make kanahemea juu juu ila nkikapa nyonyo ndo kwanza kanalia...nmechoka kukabembeleza hadi nasikia hasira kangekua kakubwa ngekapa hata vibao viwili tu vya makalio!!!!
Msaada plzzz nifanyeje???
cc: Karucee, King'ast, gorgeousmimi, geniveros na kina mama wote...
Kina baba na nyie nmewamention moyoni
Kama ukimpa formula anakunywa, hebu jaribu kukamua ya kwako. Unaweza ukakuta ni mvivu tu wa kunyonya anaona shida kuvuta kutoka kwenye chuchu ya mama anapenda chuchu inayotoa mengi kirahisi. Kuna breast pumps kwa ajili ya kukamua maziwa ya mama.
Suala hili hebu fanya kujisogeza hospital kwanza, Dk wa watoto atakupa ushauri mzuri zaidi, kumpa machakula ya kawaida mtoto wa umri huo bado sio sahihi kumbuka maziwa ya mama ni muhimu kuliko kitu chochote kwa mtoto, langu ni hilo best.
Mimi nilikataa kunyonya nikiwa na miezi miwili,mpe uji wa kutosha na hayo maziwa mengine,maombi usisahau dunia imechafuka haiko fair kabisa
Pole Ushauri wa mayele wala usiuchukue mtoto yeyote anaanza kupewa uji kuanzia miezi sita tena ule wa lishe pamoja na maji maziwa ya mama yana maji yakutosha yanapoanza kutoka pale mwanzo nakukata kabisa kiu ya mtoto, kwa wale mnaowapa watoto uji kuanzia miezi chini ya sita ni kumletea mtoto matatizo siku za mbeleni kwanza utumbo unakuwa haujaweza kumengenya kile mnacholazimisha kumpa tofauti na maziwa na huchangia maumivu ya tumbo kwa watoto na kujaa gesi cha kukushauri mtoto ukimwona anakataa kunyonya ziwa la mama ilhali maziwa yapo yanatoka hilo ni tatizo mpeleke kwa dr wa watoto atampima na atakupatia ushauri utakao kusaidia maziwa ya mama ni bora kwamtoto anaezaliwa na ukinyonyesha.mpaka miaka miwili hata miwili na nusu itakusaidia hata wewe mama mwenyewe kukaa mbali na ugonjwa wa saratani ya maziwa kwa kina mama .Wapendwa naombeni mnisaidie katika hili, huyu mtoto ashanichosha ana miezi minne tu ila hataki kabisa kunyonya, alianza kama miezi miwili hivi ikabidi wa tatu nianze kumpa maziwa ya fomula ila sasa naona kawa too much siku nzima hajaonja hata tone yupo bize ananyonya kidole tu...hapa namuona ana njaa kabisa make kanahemea juu juu ila nkikapa nyonyo ndo kwanza kanalia...nmechoka kukabembeleza hadi nasikia hasira kangekua kakubwa ngekapa hata vibao viwili tu vya makalio!!!!
Msaada plzzz nifanyeje???
cc: Karucee, King'ast, gorgeousmimi, geniveros na kina mama wote...
Kina baba na nyie nmewamention moyoni
uvivu kweli ni mvivu wa kunyonya hata chuchu ya plastic hanyonyi nmenunua chuchu yenye kijiko, nkimpa na.kijiko anakunywa...ila sasa ndo.najiuliza kwa umri huu ndo.nyonyo bye bye sio.itamuathiri?make hagusi kabisa
breast pump nnayo ila maziwa hata hayatoki asiponyonya
sante mwaya daktari wa watoto ndo alinishauri nimpe.fomula...najua.umuhimu wa maziwa ya.mama ndo maana napata mawazo ambavo hataki
Pole kwa kuchelewa kuitika wito mamii...Wapendwa naombeni mnisaidie katika hili, huyu mtoto ashanichosha ana miezi minne tu ila hataki kabisa kunyonya, alianza kama miezi miwili hivi ikabidi wa tatu nianze kumpa maziwa ya fomula ila sasa naona kawa too much siku nzima hajaonja hata tone yupo bize ananyonya kidole tu...hapa namuona ana njaa kabisa make kanahemea juu juu ila nkikapa nyonyo ndo kwanza kanalia...nmechoka kukabembeleza hadi nasikia hasira kangekua kakubwa ngekapa hata vibao viwili tu vya makalio!!!!
Msaada plzzz nifanyeje???
cc: Karucee, King'ast, gorgeousmimi, geniveros na kina mama wote...
Kina baba na nyie nmewamention moyoni
Pole kwa kuchelewa kuitika wito mamii...
- Ingekuwa ni vizuri ukinijuza kama una production ya maziwa ya kutosha?Yaani unahisi mtoto anapata maziwa na anashiba akinyonya?
- Na je hayo maziwa ya formula ukimpa anakunywa yote akashiba?
- Mara nyingi watoto wakishaanza maziwa ya formula yanakuwa na ladha tofauti na ya mama kama utamutam fulani kwahio wanachagua ladha hio hata mwanangu alifanya hivo.Maziwa ya mama yana ladha ya chakula unachokula mfano kama ukila chakula cha chumvi nyingi maziwa yanaweza kuwa salty na hasa kama huna production ya maziwa mengi.Jaribu kubadilisha misosi yako kula matunda mengi na fanya kama unajaribu kunyonyesha kwa ratiba mfano leo ule ugali na nyama,kesho samaki,keshokutwa supu ya kuku yenye mbogamboga...Na pia matunda unawea kubadili mojamoja kwa siku.Ili uone siku gani ananyonya zaidi.....
- Na kitu kingine ambacho unachoweza kufanya pia ni ww mwenye onja tone la maziwa,usisikie kinyaa mtoto ndo rutuba yake hio kama unaona ladha haikuvutii badili msosi uonje tena!!Nina shogaangu alikuwa akila matango mtoto anagoma kunyonya.
- Naomba ujaribu hivo vitu kisha ulete mrejesho mama.Kila la kheri...Kiss the baby for me!!
Bi mkubwa kama maziwa hayatoki mpaka anyonye kula vitu laini kama supu ya samaki, kongoro ya noha kama wewe huwa unatumia hiyo kitu hata kongoro ya ngombe, mtori, kunywa uji wa ulezi wa moto wautie na mafuta ya samli tatizo lenu mabinti wa siku hizi mkizaa mnataka mkitoka muwe vilevile vimodo piga hivyo vitu halafu uje ulete mrejesho hapa ukimaliza shughuli ya kulea unaruhusiwa kufanya mazoezi na kuurudisha mwili wako ule wa awali amini hivyo.
Hi Avelyn Salt
Nimekupata na nimejaribu ku andika makala yangu kwa namna rahisi kabisa ya kueleweka!!!
Nini maana ya kukataa kunyonya (Nursing strike)
Hii hutokea kwa mtoto anaye kataa kunyonya wakati hajafikisha umri wa kuacha kunyonya. Kukataa kunyonya ni dalili ya kumuonesha mzazi kuwa kuna tatizo
.
Nini kina sababisha?
Nimeanisha badhi ya sababu ambazo zinasabisha mtoto kukataa kunyonya (nursing strike)
- Maumivu ya mdomo yanayo sababishwa na kuota meno, au vidonda mdomoni au kupata maambukizi mdomoni.
- Akiwa na maambukizizo kwenye masikio (ear infection) inasababisha pressure au maumivu wakati anavuta maziwa.
- Akiwa na mafua, au kitu cha kumzuia kupumua vuzuri inafanya asipumue vizuri wakati wa kunyonya na hivyo kukosa hamu
- Kama maziwa yanatoka kidogo sana akinyonya, huwa anachoka na hivyo kukata tamaa/kuacha.
- Kubadilika badilika sana kwa ratiba ya kumnyonyesha mtoto
- Kumshtua sana mtoto pale anapo minya ziwa kwa fizi au vimeno vya maziwa, wengine hogopa na kuacha kabisa kunyonya.
- Kubadilisha sabuni ya kuoga au manukato yanayo fanya mtoto akikaa karibu na ziwa asikie vibaya au asihisi kuwa ni mama yake.
- Kubadilika kwa ladha ya maziwa kunakosababishwa na vitamin au dawa za kupanga uzazi au hata homone (kutoka ujauzito na kurudia tena hali ya kawaida- hedhi) nk
Unacho wezakufanya
Kukataa kunyonya kwa mtoto, inatokea hata kwa wamama wale ambao wapo nyumbani muda mwingi na wanapenda kunyonyesha watoto wao hivyo usiogope. Cha msingi ni kuwa mvumlivu na kujaribu namna mbalimbali za kumsaidia mtoto kwani huwa anarudi katika hali yake ya kawaida.
Mara nyingi mtoto hukataa kunyonya kwa siku kati ya mbili hadi tano hivi, halafu hupata ham kidogo kidogo. Kwa muda huo akiwa kwenye mgomo ndio unatakiwa ujitahidi kujua tatizo ili lirekebishwe arudie hali yake; ila usipojitahidi kujua tatizo hapo hukataa kabisa.
Wakati huo akiwa kwenye mgomo unatakiwa utumie pump na kumpa mtoto kwa kijiko/chupa au sirinji ya kulishia. Kumbuka, ni vizuri uendelee kukamua maziwa yako ule muda ambao mtoto angekuwa ananyonya ili yasije kukauka/kuacha kutoka hapo baadae.
Hapa ni baadhi ya njia za kufanya mtoto akikataa kunyonya (Nursing Strike)
- Jaribu Kunyonyesha wakati amelala. Utafiti umeonesha watoto wengi wanao kataa kunyonya wakiwa macho, hunyonya wakati wamelala.
- Badilisha staili ya kumnyonyesha kwani kuna watoto hawapendi kunyonya kwa kushikwa namna moja tu (wanachoka).
- Nyonyesha wakati unatembea/unazunguka zunguka kidogo hata ndani ya sebule yako. Kuna kundi la watoto wengi wanapenda kunyonyeshwa wakati mama anatembea tembea kuliko kukaa au kusimama sehemu moja tu.
- Pendelea kunyonyesha mahali penye utulivu. Hii inahusu sana watoto kuanzia miezi tano hivi kwani hupata uwoga na kujihisi hawapo salama. Pendelea sehemu isiyo na mwanga mkali au makelele ya radio au TV.
- Hakikisha mtoto anakuwa karibu sana na mama wakati wa kunyonya (skin-to-skin contact) inapendekezwa kuwa unaweza kumvua hata nguo abaki na dyper to kama inafaa. Pia hakikisha chuchu yote inakuwa mdomon kwa mtoto.
- Huwa tuna shauri mama akitoka kwenye mishuhuliko/kazini awe na utaratibu wa kuoga kabla ya kunyonyesha; hii hufanya mama ababikie kuwa natural kwa mtoto na maziwa yanakuwa kwenye joto la kawaida.
- Kwa matatizo kama ya masikio au Vidonda mdomoni ni vizuri uonane na daktari wako kwa ushauri na kuchunguzwa vizuri.
Ni vizuri kukumbuka kuwa motto chin ya mwaka mmoja hawezi kukataa kunyonya eti kwa kuwa wakati wake wa kuacha kunyonya umefika. Sikuzote ukiona hivyo ujue ni tatizo na klinahitaji kufanyiwa ufumbuzi.
Pia ni vizuri kujua kuwa, mama akipata ujauzito maziwa hubadilika ladha kwa sababu ya homone na mara nyingi watoto hukataa kuyanyonya.
Asanteni