GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Zanzibar na Tanga ni kati ya mikoa yenye idadi kubwa sana ya waislamu. Hayo yasingewezezekana kama Waislamu wangekuwa wanakazana kuwaambia watoto wao waswali huku wao wakifakamia "kitimoto"
Ni mtu mzima pekee anayeweza kumwelewa Daktari mvuta sigara anayewahamashia watu wasivute sigara wakati yeye hawezi kuwa na utulivu bila kuvuta.
Ni mtu gani anayeweza kukubaliana na Mchungaji anayehubiri kuwa "ulevi" ni dhambi lakini yeye hakai mbali na bapa la Konyagi?
Watoto ni watu hodari sana kujifunza kwa kuona. Ukiwa utafanya tofauti na unavyowaelekeza, watachukulia kuwa hicho unachowakataza kina upekee usiotaka waufaidi. Na kama ulikuwa unawahamasisha wafanye usichokifanya, watachukulia kuwa hakina manufaa, ndiyo maana wewe mwenyewe hufanyi hayo.
Wahenga wakashauri, kuwa kijana anapotaka kuoa, asimwoe binti ambaye yeye (kijana mwoaji) hayuko tayari "kumwoa" mama yake. Wanaamini, kuwa tabia ya binti kwa kiasi kikubwa, huakisi tabia ya mama yake(japo si mara zote). Hiyo pia inaweza ikawa sawa na kwa upande wa vijana wa kiume. Tabia zao zinaweza kuendana na za baba zao (japo si mara zote). Ndiyo maana miaka ya nyuma, kwa baadhi ya makabila, wazazi husika kuchunguza familia watoto wao wanakotaka kuoa au kuolewa.
Nimeangalia clips za msiba wa Jenerali Ogolla, CDF wa Kenya aliyekufa kwa ajali ya ndege.
Watoto wake wanaonekana walilelewa na wakaleleka! Inawezekana mengine "wameyakuza", lakini, vyo yote vile, inaonekana Jenerali Ogolla alikuwa "mwanaume"
1. Alimpenda mke wake kiasi cha watoto wake kujua kuwa baba yao anampenda mama yao vilivyo
2. Aliwaambukiza watoto wake tabia ya usomaji Biblia na vitabu vingine. Ingawa watoto wake walikuwa wameshakuwa watu wazima wenye familia zao, bado alikuwa akifanya nao mashindano ya usomaji wa Biblia.
3. Alikuwa mchapa kazi wa kupigiwa mfano. Hata watoto wake wanaonekana wana hizo tabia za uchapaji kazi.
Wakati fulani, wakati akiwa kazini, Jenerali Ogolla alitumia kipindi kisichozidi miezi sita kujifunza lugha ya Kifaransa na akafanikiwa.
Hiyo isingewezekana kwa mvivu. Angetoa "excuse" kuwa ajira inambana.
Kama una watoto, jitahidi kuishi maisha yatakayokua mfano kwao.
Kila kitu wakionacho ukikifanya kina athari kwao.
Ukimpiga mama yao, hawatafurahia, na hawatataka waje kufanya hayo baadaye watakapokuwa watu wazima. Lakini kwa kuwa wakionacho hugeuka kuwa msingi wa maisha yao, watajikuta na wao wanakuja kufanya yao hayo maishani mwao.
Ukimdharau mumeo, ujiandae kuja kupokea kesi za binti zako kutoka kwa waume zao kuwalalamikia kuwa wanawadharau. Unavyomfanyia baba yao ndivyo unavyowafunza binti zako kuja kuwafanyia waume zao.
Kamwe watoto wako wasijue kuwa wewe ni "mlevi" ikiwa hupendi waje kuwa "wanywaji".
Kila kitu watoto wako wakionacho ukifanya ni matofali yanayojenga tabia yao ya kesho.
Ishi nao kiusahihi ili kesho usije kufadahaishwa na usiyoyatarajia kutoka kwao.
Jifunze kwa hayati Jenerali Ogolla wa Kenya.