Tulizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 848
- 664
.Je ni kweli kwamba mkipata mtoto huifanya ndoa yenu iwe imara zaidi? Mi binafsi nachukulia kama mipango ya Mungu tu, labda watafanikiwa mbele ya safari.
Ndugu yangu, nakubaliana na wewe ya kuwa kupata mtoto wako binafsi ni mipango ya Mungu, Ukiacha wale wanaoharibu kizazi kwa kutoa mimba wakati wa ujana halafu baadaye wanatafuta mtoto na kukosa.
Furaha ya mtoto inakujaje? Ukiwa na akili timamu ambayo haijaharibiwa na kilevi mtoto au watoto watakukumbusha daima ya kuwa upende au usipende baba na mama mnawajibika kwa 100% kwa wao kupumua na kuona jua kesho yake. Hivyo basi.. ukiweza kutimiza wajibu huu kwa uwezo wako..unajisikia ufahari.. na moyo wako unakuwa na amani kwani unaona umesaidia malaika wasio na mbele wa nyuma. Kwa upande mwingine kwa sababu watoto ni zao la watu wawili..wanaonekana kama daraja la muunganiko wa mahusiano..
Kuhusu furaha hii kama inawezekana kupatikana kutokana na mtoto wa ku-adopt.. hili linategemea na saikolojia ya wazazi wote wawili na mazingira.. Kama nilivyosema..kama furaha yenu itakuja kwa kujiona ufahari ya kuwa kuna kiumbe kinawategemea kwa asilimia 100% kuona jua ..basi mtakuwa na furaha hata kama mta-adopt mtoto, lakini kama mnashindwa kundoa mawazo ya kuwa hakuna tofauti kati ya biological child na yule wa asili yenu..basi hamtaweza pata hiyo furaha.
..Lakini ukweli utabaki mtoto ni mtoto..kwani ni malaika anayetegemea mtu mwingine iwe yule aliyemleta au yule aliye m - adopt.