Mtoto kuanza kucheza tumboni

Sperience

Member
Joined
Dec 27, 2013
Posts
5
Reaction score
1
Heri ya mwaka mpya wadau, Jaman naombeni msaada nina ujauzito wa week14 nilienda kufanya ultrasound juzi mtoto wangu ameonekana akicheza yaan anaruka sio mchezo, dr akinibonyesha mahali akimwangalia kwenye screen anamuona anavyorusha miguu na mikono, mimi sisikii chochote ni kwenye ultrasound tu ndio ameonekana. je ni sawa? Msaada jaman nimepatwa na wasiwasi japo dr anasema sio ajabu lakini mm mama mtu nikilinganisha na wenzangu wengi husema kuanzia miezi mi5.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usijari. Kwani hata wewe nini kilikupeleka kwa doctor?
 
Ukifikisha kuanzia miezi mitano na kuendelea utasikia vipepsi vya kutosha na mateke .
 
Dogo anaogelea na kujimwayamwaya kwenye amniotic fluid. Kati ya wiki ya 16 mpaka 24 ya ujauzito utaanza kusikia hayo mateke na masumbwi. Kitaalamu inaitwa, "Quickening ".
 
Mtoto wa kwanza huanza kucheza wiki 15-25 lakini wapili huanza wiki 13.
 
mbona kawaida mkuu, mtoto anaweza kuanza kucheka kati ya wiki ya 13-25, ila kwa wale ambao ndio mimba ya kwanza au wanene sana ndio huwa wanachelewa kuhisi mtoto anavyocheza mkapa wiki ya kati ya wiki ya 15-18.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…