Mtoto kuanza kuota meno ya juu kuna shida yeyote kiafya?

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
1,259
Reaction score
1,056
Habari za leo ndugu zangu wapendwa? Ni matumaini kuwa mpo safi kabisa. nimekuja hapa kwenye hili jukwaa nikiwa nina shida moja inayonitatiza.
jana nilikuwa nampa chakula mwanangu (ana miezi 7 na siku kadhaa), sasa wakati nampa nikaona kuwa ameanza kuota meno ya juu badala ya meno ya chini kama ilivyokuwa kawaida.

Hali hii nilishangaa na hata baadae nikamwambia mke wangu ambae nae pia alishangaa na hakuwa na majibu. Sasa nimeleta hii mada hapa kwenu mnipe ushauri kama kutakuwa na shida yeyote katika maendeleo na ukuaji wa mwanangu mpendwa. Nitashukuru sana kwa michango yenu.

NB: Kama hautakuwa na mchango wa maana tafadhali pita wima,

this is serious case.
najua hii ilitakiwa kwenda JF doctor ila pia najua huku kuna wadau wengi, please mods msiihamshe hii post, natanguliza shukurani za dhati
Cc; MziziMkavu, Mtambuzi, faizaFoxy na wengine
 
Kwanza nikupe hongera kwa kuitwa baba mkuu.
Eiyer unakumbuka ile siku ulienda kumzika rafiki yako?? Unakumbuka zile story za wale wazee??
 
Last edited by a moderator:
Hakuna shida. Mm hapa pia nilianza meno ya juu. Mama aliniambia na mtt wa kaka pia alianza na meno ya juu
 
Sidhani.

Nadhani ni moja tu ya peculiarities za watoto. Miss lady wangu alianza kutembea akiwa na miezi sita na hakuwahi kutambaa.

Nilipoulizia nikaambiwa hakuna tatizo lolote lile kwani wapo watoto wa hivyo.
 
Kawaida, mi kuna mtoto nlimuona kaota haya meno ya kwenye kona sijui ndo yanaitwa canivo nini nmesahau, tena ya juu kabla ya kuota meno ya mbele
 
Ni kawaida tu mie mwenyewe nilianza kuota meno ya juu wakawa wananiita kigego. Katika imani za wazee wetu zamani ni kuwa mtoto akianza kuota meno ya juu ni mchuro huyo mtoto au analeta mikosi. . .hivyo wakawa wanauliwa enzi hizo - hayo nilikuwa naambiwa na koko wangu kwakuwa mie nami nilianza hayo ya juu
 
Ni kawaida kabisa, mtt wangu alitanguliza meno ya juu ila yuko poa ni kawaidaaaa
 
mimi mtoto wangu wa miaka 4 na nusu kang'oka meno mawili ya chini na mengine yameota kwa haraka na kuziba yale mapengo. hakuendelea tena kung'oka baada ya hapo. sijui akifika umri wa kung'oka meno yatang'oka kwa mara ya pili. iam indeed puzzled! mwenye kujua hiki kitendawili naomba anisaidie kutegua. yaani hili ni suala la ajabu ambalo sijawahi kulishuhudia.
 
inaonekana unaenda sana kwa waganga ndio maana hali kama hiyo imekupata.
 
Habari za leo ndugu zangu wapendwa? Ni matumaini kuwa mpo safi kabisa. nimekuja hapa kwenye hili jukwaa nikiwa nina shida moja inayonitatiza.
jana nilikuwa nampa chakula mwanangu (ana miezi 7 na siku kadhaa), sasa wakati nampa nikaona kuwa ameanza kuota meno ya juu badala ya meno ya chini kama ilivyokuwa kawaida.

Hali hii nilishangaa na hata baadae nikamwambia mke wangu ambae nae pia alishangaa na hakuwa na majibu. Sasa nimeleta hii mada hapa kwenu mnipe ushauri kama kutakuwa na shida yeyote katika maendeleo na ukuaji wa mwanangu mpendwa. Nitashukuru sana kwa michango yenu.

NB: Kama hautakuwa na mchango wa maana tafadhali pita wima,

this is serious case.
najua hii ilitakiwa kwenda JF doctor ila pia najua huku kuna wadau wengi, please mods msiihamshe hii post, natanguliza shukurani za dhati
Cc; MziziMkavu, Mtambuzi, faizaFoxy na wengine

Mkuu pole kwa mshtuko.Je umeangalia hayo meno sio ya plastik? Ila kama ni meno ya kweli na sio ya plastik ujue umerithi matunguli au wewe au mkeo alikuwa anaenda kwa mganga.Cha kufanya piga magoti utubu na kukana mila zenu zote na kisha ukizaa mtoto mwingine hiyo haitatokea.
 
Kwa kweli hi kitu mdau usiogope lakini wazee wengi walisema mtoto akiota meno ya juu ni uchuro yaani kuna possibility wazazi wake wote wawili wakafa akiwa bado na umri mdogo yaani chini ya miaka 12 swali je nyinyi mliosema kawaida je ulishaona mtoto kaota meno ya juu kwanza na akakuwa hadi mtu mzima wazazi wake bado wakiwa hai mi kuna nilioshuhudia wazazi wakifariki mazingira ya ajabu hadi ikawa gumzo kijijini Kuwa ni uchuro wa mtoto wao kuota meno ya juu kwanza lakini mleta mada usiogope unaweza kwenda kanisani au msikitini kutokana na imani Yako kuomba Mungu avunje roho zote za hayo mapokei ili uishe vizuri na uzima wewe na familia yako
 
mwambie aende church
 
Mhh. ukistaajabu ya malimwengu.
 
mama yake alilia sana hapa jirani akashauriwa amtupe bibi alichachamaa akasema atakua! vijana wanapanga foleni kumtafuta angetupwa je!
na wala hakuna kilichotokea haya sasa naambiwa hapa na huyu dogo ana miaka tisa. piga menyu mwandalie ada ya skuli dogo kwa huo upekee wake anaweza kuwa Julius K Nyerere sio hawa wasanii
 
Back
Top Bottom