Mtoto kucheua maziwa puani

Mtoto kucheua maziwa puani

Tricker

Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
95
Reaction score
25
Naombeni kuelimishwa,mtoto wa chini ya mwezi mmoja kucheua maziwa na mengine kutokea puani inaweza kusababishwa na nini?Je ni hali ya kawaida au ni tatizo kubwa?
 
Wanasema ukimpa mtoto mchanga maziwa au nyonyo ni lazima umweke kama unamsimamisha huko tumbo lake likiwa limelalia kifua chako au tuseme bega lako huku unampiga piga kidogo kidogo kwa kiganja cha mkono wako mgongoni kwake,
unafanya hivyo hadi usikie amecheuwa, na hapo unakuwa na uhakika kuwa maziwa yameshashuka tumboni hawezi kucheuwa tena.

Usipofanya hivyo kuna hatari ya mtoto kupaliwa maziwa au yakaingia kwenye njia ya hewa hivyo akapata shida.

Huu niliosema ni ulezi wa kizamani, kwa miaka hii sijui vizuri, MziziMkavu atanisaidia hapa.
 
Naombeni kuelimishwa,mtoto wa chini ya mwezi mmoja kucheua maziwa na mengine kutokea puani inaweza kusababishwa na nini?Je ni hali ya kawaida au ni tatizo kubwa?
Mwanangu pia ana tatizo hilo ulipata dawa
 
Watoto wenu mnawapa vile vidude vya kunyonya mdomoni kwa kizungu dummies?! Vile msiwape sio vizuri. Sijajua uhusiano wake hapa lkn nadhani vitakua vinaharakisha matatizo ya dezine hiyo
 
Back
Top Bottom