Ni kitu gani kitamsaidia mtoto kujifunza kingereza,je awe anaangalia tamthilia za kingereza zilizotafsiliwa,kusoma hadithi za kingereza au kuangalia katuni? Naomba pia kujua kama kuna kifaa ambacho kime include games tu maana hawa watoto wetu siku hizi wanapenda sana simu sasa simu sio nzuri mtoto anaweza jifunza na visivyofaa.
Mtoto ana miaka mingapi?
Kama bado hajaanza shule na ni mdogo inabidi wewe mwenyewe ujue kiingereza (,kama bado) ili uwe unazungumza naye tangu akiwa mdogo. Atakuwa akiwa anajua.
Pia jaribu kumtafutia nanny ambaye anazungumza hiyo lugha.
Kama yupo shule mpeleke shule wanazotumia hiyo lugha kwa %kubwa.
Penda kuwa na mazungumzo nae kwa lugha unayopenda aijue + katuni (ukianzia na zile basics nikimaanisha za namba, herufi n.k) polepole ata anza kuongea na kuelewa.
Mimi wangu nimewaongelesha kiingereza na kiswahili toka wanaanza kuongea wanajua lugha mbili na bado hawajaanza shule.