Mtoto kukataa kula

uroto

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2015
Posts
442
Reaction score
227
Habari za mda huu wana jf doctor


niende kwenye mada ni kwamba nina mtoto wa kike wa mwaka mmoja na mwezi mmoja

tatizo mtoto hataki kula,tumemjaribu kila aina ya chakula,ila ukimrisha anatema,anapenda kunyonya

huu ni mwezi wa2 sasa,hospitally tumeenda ila bado habadiliki,imefikia hata akiwa anatembea anakuwa anapepesuka sasa yaani hana nguvu

msaada eenu wandugu
 
Habari za mda huu wana jf doctor


niende kwenye mada ni kwamba nina mtoto wa kike wa mwaka mmoja na mwezi mmoja

tatizo mtoto hataki kula,tumemjaribu kila aina ya chakula,ila ukimrisha anatema,anapenda kunyonya

huu ni mwezi wa2 sasa,hospitally tumeenda ila bado habadiliki,imefikia hata akiwa anatembea anakuwa anapepesuka sasa yaani hana nguvu

msaada eenu wandugu
 
Mwambie mama yake ajitahidi kumnyonyesha na pia ajaribu kuwa anamkaba,hata mimi alikuwa anasumbuwa nashukuru sasa hivi walau anakula angalau.
 
Ingekua mimi ningemuachisha kunyonya angekula tu maana njaa inamuuma na nyonyo hakuna.

Usimkabe aisee ni hatari
 
Jaribu kumuwekea finger foods. Hivi ni vyakula kama nyama za kavu bila mchuzi, carrots, viazi, mihogo ya kuchemsha na matunda kama zabibu lakini zikatwe katikati, machungwa na machenza yaliyomenywa.
Weka sehemu anayofikia, akisikia njaa atachukua.

Kuna watoto ambao hawapendi routine ya chakula lakini wanaokoteza huku wakiwa wanaendelea kucheza.
 
Pole sana mkuu,aisee usipokuwa imara atakusumbua sana.

Mtoto wa dada yangu alikuwa hivyo ss yy ilikuwa zaidi maana mpaka anafikisha miaka 2.5 alikuwa hali chochote yy ni kunyonya tu hata kutembea alikuwa hatembei na ukimuangalia ngozi ilikuwa nyororo ile ya kung'aa km utapimlo yaani haina hata dalili ya vinyweleo mpaka ikabidi bimkubwa aje ndo sister akampeleka mtoto kwa bibi ilimradi aache kule kunyonya.

Siku za mwanzo hali ilikuwa tete kwa bimkubwa ilibidi Azam embe zisikatike ndani hasa usiku ila tunamshukuru Mungu alipoanza kula hali ilibadilika na sasa ana miaka 4 anakimbia na yuko safi tena ni kikorofi hatari.
Mkuu chakula ni dawa pia mkazanie sana.
 
Mkabe kwa upendo sio kwa hasira, wa kwangu tulishirikiana baba na mama kumkaba kwa upendo, sasa amezoea na anakula kama mchwa
 
Mwambie mama yake ajitahidi kumnyonyesha na pia ajaribu kuwa anamkaba,hata mimi alikuwa anasumbuwa nashukuru sasa hivi walau anakula angalau.


anamnyonyesha tena sana tu,ila chakula ndo anatema
 
Ingekua mimi ningemuachisha kunyonya angekula tu maana njaa inamuuma na nyonyo hakuna.

Usimkabe aisee ni hatari


kuhusu kumwachisha,tumepanga had atimize mwaka na nusu
 


wakwangu pia anakunywa sana juice za embe zile za Azam,anapenda kuliko kula
 
Acha kumpa juisi, pipi na punguza kiasi whole milk unachompa.

Chagua kumpa matunda na kumlisha wakati au mida familia inakula.
 


Nsshukuru ntafanyia kazi huu ushauri
 
Acha kumpa juisi, pipi na punguza kiasi whole milk unachompa.

Chagua kumpa matunda na kumlisha wakati au mida familia inakula.


sawa ntaacha kumpa pipi,biskuit na nimzoeshe matunda
 
asee mkabe Hugo usimuonee huruma,wifi angu alikua anamkaba wakati Wa uji mpaka unaisha ,bila nguvu hawali hawa .
 

******
Ndugu Sky Eclat na nyote, ahsantenii kwa ushauri mzuri, je kama ana miaka 10 lakini ana shida kama hiyo nifanyeje, maana hospitali tuliambiwa atabadirika lakini tumempa kila aina ya matunda na kila aina ya vyakula hali haibadiriki, hata vyakula vizuri kiasi gani.Natamani ungeniruhusu niwe nakuuliza/kukueleza mara kwa mara maendeleo yake, Mungu awabariki wachangiaji nyote.
 
Unajua shida hii mara nyingi inawakumba watoto wa familia bora ila huwezi kuikuta kwa wale watoto ambao msosi ni gombania goli,hebu karibu kumpeleka likizo mazingira tofauti na hapo.

Hapa tunajaribu kushare uzoefu tu coz tayari hospitali ushaenda na matokeo bado ni negative.Kuna watoto ambao hawapendi kula kabisa hivyo bila kuwa mkali utasumbuka sana nakumbuka nilikuwa na jirani yangu baba na mama mtoto anawagomea kabisa kula hivyo nasubiriwa mm nitoke kijiweni SAA 5usiku maana bachelor narudi muda naotaka,then nawakuta wananisubiri niwalishie mtoto na nikifika bila ukali namlisha habakizi hata kidogo.Hiyo hebu jaribu kuwa mbunifu tu unaweza pata solution.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asubuhi mpigishe mswaki na whitedent atakula tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…