Mtoto kupungua damu

Mtoto kupungua damu

mama fulani

Member
Joined
Aug 10, 2013
Posts
24
Reaction score
7
Habari za mida hii wadau? mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miezi kumi na moja sasa. Mwanangu alipofika miezi miwili nilimuanzisha maziwa ya ng'ombe ndipo shida ilipoanza alikua anapata homa kali nilipompeleka hospitali baada ya vipimo ikagundulika damu na madini chuma yamepungua nakumbuka alikua na damu nane kipindi hicho alikua na miezi miwili na Doctor akaniambia maziwa ya ng'ombe ndo yamesababisha hyo shida. Sasa tatizo lililopo mpaka sasa damu haiongezeki vzuri nadhani na uzembe wa kutompa dawa za damu kwa wakati sasa naombeeni ushauri ndugu zangu kwa umri wake ni vyakula gani vitamsaidia kumuongezea damu kwa haraka haijawahi kupungua zaidi ya nane tisa mpaka kumi msaada jamani ulezi wa mtoto wa kwanza ni mgumu.
 
Fuata ushauri wa daktari na utumie dawa ya kuongeza damu ipasavyo!Matunda na mbogamboga kama zabibu(au juisi ya zabibu) ni mazuri kwa kuongeza damu na madini ya iron,cornproducts,nyama nyekundu pamoja na maini inasemekana pia yanaongeza damu,mayai n.k
Ni kweli alivyosema daktari maziwa yanazuia uptake of iron..kwahio ni vyema ukiepuka kumpa wakati wa milo au ukimpatia dawa!
 
Chukua matembele yaoshe vizuri kisha twanga kamua juice yake, ipashe kidogo kuua vijidudu, ongeza chumvi kidogo then mpe kutwa mara tatu utapata matokeo mazuri
 
Back
Top Bottom