mama fulani
Member
- Aug 10, 2013
- 24
- 7
Habari za mida hii wadau? mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miezi kumi na moja sasa. Mwanangu alipofika miezi miwili nilimuanzisha maziwa ya ng'ombe ndipo shida ilipoanza alikua anapata homa kali nilipompeleka hospitali baada ya vipimo ikagundulika damu na madini chuma yamepungua nakumbuka alikua na damu nane kipindi hicho alikua na miezi miwili na Doctor akaniambia maziwa ya ng'ombe ndo yamesababisha hyo shida. Sasa tatizo lililopo mpaka sasa damu haiongezeki vzuri nadhani na uzembe wa kutompa dawa za damu kwa wakati sasa naombeeni ushauri ndugu zangu kwa umri wake ni vyakula gani vitamsaidia kumuongezea damu kwa haraka haijawahi kupungua zaidi ya nane tisa mpaka kumi msaada jamani ulezi wa mtoto wa kwanza ni mgumu.