Kwanza muhimu kufahamu kuwa mtoto wa mwaka mmoja hua anapoteza hamu ya kula, Huanza kuchagua vyakula atakavyokula na akitafuna chakula kidogo huzungusha kichwa pembeni kuashiria kuwa hataki kula tena. Walezi wanaomlea huanza kufikiri labda mtoto anaumwa lakini ukweli ni kuwa kuna sababu nzuri ya mabadiliko hayo ambayo ni kupungua kwa ukuaji wa mtoto ambapo mwili wa mtoto huitaji chakula kidogo kulinganisha na miezi ya nyuma.
Ni makosa kumlazimisha mtoto wako ale chakula wakati hataki, na pia kumbuka jinsi unavyotumia nguvu sana kumlazimisha ndio jinsi anavyoendelea kuchukia icho chakula. Watoto wa mwaka mmoja huwa hawatabiriki wakati wa kula, kwani anaweza akala chakula anachokipenda asubuhi halafu asile tena chakula kingine mpaka siku inaisha.
UFANYAJE ILI MTOTO WAKO APENDE KULA?
Mletee vyakula mbalimbali vyenye virutubisho na muache achague anachokipenda. Hakikisha vyakula hivyo vina ladha tofauti na visifanane.Kama bado hataki mtayarishie chakula halafu ukihifadhi na utampa kipindi akiwa amepatwa na njaaUsimpe mtoto vitu kama pipi na biskuti kwa sababu atapata nishati peke yake bila virutubisho(empty calorie foods) na pia atapoteza hamu ya vyakula vyenye virutubisho.Usimlazimishe ale muda unaotaka wewe mleziNa ili mtoto wa mwaka mmoja aendelee kukua anahitaji vyakula kamaNyama, samaki na mayaiMaziwaMatunda na mbogambogaVyakula vya mbegu na jamii ya mizizi kama viazi
VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA
Usimpe mtoto vyakula vyenye viungo vingi na vyenye harufu sana, pia epuka kumpa vyakula vyenye chumvi au sukari nyingi.Epuka vyakula vinavyoweza kumfanya mtoto apaliwe. Hakikisha umemsagia chakula au umekata katika vipande vidogo vidogo.Pia mfundishe mtoto mtoto kunywa maji kwenye kikombe. Kumbuka pia kipindi hiki mtoto hupunguza uitaji wa maziwa.