Mtoto kutopenda kula, nini kifanyike?

Mtoto kutopenda kula, nini kifanyike?

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
11,261
Reaction score
17,202
Wadau nina mtoto ana mwaka mm o j?? na nusu ni mvivu sana wa kula.. Ikifika muda wa chakula ni ugomvi.. Hata afya yake imeanza kudhoofu.. Nitashukuru kwa Msaada wa mawazo.
 
We are suffering from the same problem. Nasubili wataalam watupe ushauri.
 
Unampa chakula gani na kwa ratiba gani? Tuanzie hapo.
 
Nenda muone daktari inawezekana Kuna tatizo lakini pia jaribu kulazimisha.mimi mtoto wangu ana almost 3 years now anakula Chakula kila saa imebidi tumuwekee ratiba kwakweli.
 
Unampa chakula gani na kwa ratiba gani? Tuanzie hapo.

Chakula cha kawaida tu mkuu...mara nyingi katika ile milo mitatu mikuu huwa tunajumuika wote ingawa hapo katikati huwa anapata chochote.. Na isitoshe siku za kazi huwa anabaki na msichana wa kazi.
 
hilo tatzo alikua nalo pia mwanangu ambae ana 1yr na 3 months, gafla ilianza kugoma kula, akawa hali chochote.. ikitokea kala anakula kidogo.. nkaanzisha kumpa maziwa ya lactogen, kidogo akawa anakunywa.. juz juz nilishauriwa kumpa dawa za kuongeza ham ya kula.. kuna dawa tukaanza nayo.. aisee saiv mtoto anakula balaa anamaliza kias chote anachowekewa.. jaribu na wewe kutumia dawa za kuongeza ham ya kula.
 
Zinaitwaje hizo dawa mkuu
 
Asante kwa ushauri mkuu..
 
Binti yangu pia anahilo tatizo la kutopenda kula mpaka nina wasiwasi siku mama yake atakapolazimika kumuacha na mtu mwingine zaidi ya mama yake itakuaje manake wakati wa kula ni ugomvi mkubwa
 
Wadau nina mtoto ana mwaka mm o j?? na nusu ni mvivu sana wa kula.. Ikifika muda wa chakula ni ugomvi.. Hata afya yake imeanza kudhoofu.. Nitashukuru kwa Msaada wa mawazo.

Kama wewe ni wa Dsm nenda pale kisutu kuna dokta bingwa wa watoto kama ni tatizo la kiafya utapata suluhisho na kama sio tatizo la kiafya atakuelekeza vyakula vya kumpa na mpangilio wake.. kuwa makini sana kuwapa watoto wa umri huo dawa ovyo ovyo bila kupata maelekezo sahihi kutoka kwa daktari.
 
Kwanza muhimu kufahamu kuwa mtoto wa mwaka mmoja hua anapoteza hamu ya kula, Huanza kuchagua vyakula atakavyokula na akitafuna chakula kidogo huzungusha kichwa pembeni kuashiria kuwa hataki kula tena. Walezi wanaomlea huanza kufikiri labda mtoto anaumwa lakini ukweli ni kuwa kuna sababu nzuri ya mabadiliko hayo ambayo ni kupungua kwa ukuaji wa mtoto ambapo mwili wa mtoto huitaji chakula kidogo kulinganisha na miezi ya nyuma.

Ni makosa kumlazimisha mtoto wako ale chakula wakati hataki, na pia kumbuka jinsi unavyotumia nguvu sana kumlazimisha ndio jinsi anavyoendelea kuchukia icho chakula. Watoto wa mwaka mmoja huwa hawatabiriki wakati wa kula, kwani anaweza akala chakula anachokipenda asubuhi halafu asile tena chakula kingine mpaka siku inaisha.

UFANYAJE ILI MTOTO WAKO APENDE KULA?

Mletee vyakula mbalimbali vyenye virutubisho na muache achague anachokipenda. Hakikisha vyakula hivyo vina ladha tofauti na visifanane.Kama bado hataki mtayarishie chakula halafu ukihifadhi na utampa kipindi akiwa amepatwa na njaaUsimpe mtoto vitu kama pipi na biskuti kwa sababu atapata nishati peke yake bila virutubisho(empty calorie foods) na pia atapoteza hamu ya vyakula vyenye virutubisho.Usimlazimishe ale muda unaotaka wewe mleziNa ili mtoto wa mwaka mmoja aendelee kukua anahitaji vyakula kamaNyama, samaki na mayaiMaziwaMatunda na mbogambogaVyakula vya mbegu na jamii ya mizizi kama viazi

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA

Usimpe mtoto vyakula vyenye viungo vingi na vyenye harufu sana, pia epuka kumpa vyakula vyenye chumvi au sukari nyingi.Epuka vyakula vinavyoweza kumfanya mtoto apaliwe. Hakikisha umemsagia chakula au umekata katika vipande vidogo vidogo.Pia mfundishe mtoto mtoto kunywa maji kwenye kikombe. Kumbuka pia kipindi hiki mtoto hupunguza uitaji wa maziwa.
 
asante sana umenisaidia sana
 
Kisutu sehemu gani mkuu, tusaidie tukamuone, hii shida sasa hata wadada wanakimbia kazi kila siku
 
Back
Top Bottom