Mtoto kuzaliwa baada ya miezi 11

Mtoto kuzaliwa baada ya miezi 11

kuwota

Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
79
Reaction score
28
Wakuu habari za wakati huu? Je inawezekana Mtoto akazaliwa baada ya miezi 11 na akawa salama kabisa? Je hili jambo ni la kushangaza au huwa linatokea?
 
Kwa kawaida mtoto huishi katika tumbo la mama kwa muda wa miezi 9 sawa na wiki 37 mpaka wiki 40 ambazo ni sawa na miez 10 japo wengine huzaliwa chini ya wiki 37 ambao huitwa watoto njiti. Kuzidi miezi 11 sina hakika sana, nakushauri uonane na madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwaajili ya uchunguzi zaidi.
 
Wakuu habari za wakati huu? Je inawezekana Mtoto akazaliwa baada ya miezi 11 na akawa salama kabisa? Je hili jambo ni la kushangaza au huwa linatokea?
ni la kushangaza na huwa linatokea pia.

kama kuna mjamzito hilo limemkuta aende hospitali waone kama kuna ulazima wa kumwanzishia uchungu mtoto atoke au suluhisho jingine.

Pia kumbuka mtoto muda huo anaendelea kukua, so kadri siku zinavyozidi kuongezeka na yeye anazidi kukua, hivyo kufanya uwezekano wa kuzaliwa kwa njia ya kawaida kuzidi kupungua maana huenda njia isitoshe.
 
Sio kawaida.Huenda mama kakosea kuhesabu siku.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Inawezekana pia kama hakuhudhulia cliniki anaweza kujidanga kupiga hesabu ya siku za mimba, kama ulisha wahi kusikia mtu amejidanganya kuwa ni mjamzito wakati sio mjamzito!. Hayo yote yanawezekana!.
 
Mahesabu ya mama hayako sawa na bila shaka hakuhudhuria clinic vinginevyo wangegundua kupitia vipimo kiumbe mtarajiwa ana miezi mingapi tumboni.

Sio kawaida.Huenda mama kakosea kuhesabu siku.
 
Back
Top Bottom