Mwaka Jana kuna mdada nilimpatia ujauzito, mimba ilikaa miezi kumi na alipojifungua mtoto alitoka kaishafariki na alikuwa na kitovu cha kijani. Ila kabla hajajifungua walipima mapigo ya moyo mtoto yalikiwa yapo sawa. Nesi anasema labda dada huyo alitumia Dawa za kienyeji au alikula mboga za majani bila kuosha vizuri hivyo akala na chemicals, ila yeye anasema hajawahi kutumia Dawa za kienyeji ila pia binti huyo amekeketwa hilo linaweza kuwa tatizo?