Mtoto kuzaliwa na manjano.

Mtoto kuzaliwa na manjano.

Dah imani hizi bwana. May be .......hatuwezi kubisha tu maana kwa imani zetu za kidaktari ni vitu tofauti nikipata muda nitafafanua nini kinatokea mwilini mpaka mtoto awe wanjano. Ila lisemwalo lipo hata kama unaona halina proof kisayansi. Mimi japo ni daktari lakini nishawahi kutibiwa pumu na ikapona kwa namna ambayo haina logic lakin nilipona. I respect them
 
Baada ya kuambiwa hivyo huko kwenye vitenge, nilirudi mtaani kupata maoni kwa akina mama watu wazima lakini nao walisema nguo za njano na maembe sio mazuri. Kwahiyo hizi imani zipo sana mkuu. Hapo mtaani kwako jaribu kufuatilia unaweza kuyakuta haya.
Mkuu kitabibu hicho kitu hakuna.

Nazungumza kama medical personnel
 
Habari zenu wakuu.
Mke wangu ana ujauzito wa miezi 7. Juzi tulikwenda kufanya manunuzi ya vitu kama vile vitenge,kanga na baadhi ya vyombo lakini yote ni maandalizi ya kumpokea kijacho.

Tupo kwenye duka la vitenge na kanga wife wakati anachagua alichagua baadhi ya vitenge na kanga zenye rangi ya njano. Muuzaji alikua ni mama mtu mzima(age go) alimwambia wife kua hata mimi ni mama sikushauri mwanangu uchukue hizi nguo zenye rangi ya njano maana utaleta manjano kwa mtoto.
Nilishtuka nikamuuliza mama je hata matunda kama embe nayo yanarangi inayofanana na njano, akasema maembe asile kwa kipindi hiki.

Hapa naomba ushauri na udhoefu wenu juu ya manjano hasa kwenye nguo za njano wakati mama anajifungua na ulaji wa maembe. Maana wife alikua anakula sana maembe ila ameacha juzi baada ya kupewa darasa na huyo mama wa vitenge.
Hakuna uhusiano. Hicho anachokisema huyo muuzaji aidha ametengeneza yeye kichwani au amewekewa kichwani na wala hakipo nje ya kichwa chake.

Kuhusu manunuzi ya nguo za mtarajiwa ni vyema manunuzi yafanyike mara mgeni anapowadia, kama ni issue ya fedha ni vyema kuweka hiyo pesa mpaka muda utakapowadia. Ila maandalizi ya khanga na vitenge viwili vitatu ni lazima ila pale siku zinapokuwa jirani.
 
Dah imani hizi bwana. May be .......hatuwezi kubisha tu maana kwa imani zetu za kidaktari ni vitu tofauti nikipata muda nitafafanua nini kinatokea mwilini mpaka mtoto awe wanjano. Ila lisemwalo lipo hata kama unaona halina proof kisayansi. Mimi japo ni daktari lakini nishawahi kutibiwa pumu na ikapona kwa namna ambayo haina logic lakin nilipona. I respect them
Asante sana mkuu.
Mimi sio daktari lakini kwakusikia mtaani na kuelimishwa nina abc za manjano lakini darasa lako bado nalihitaji sana.

Yule mama wa vitenge nilimuuliza kua manjano kwa kichana vina uhusiano gani na mama mjamzito kula maembe au kutumia nguo zakijani wakati wa uzazi? Alinijibu mwanangu mimi na wewe hatuwezi kubishana kwenye mambo ya uzazi. Kua anachoniambia anakijua na hata wauguzi hicho kitu wanakifahamu.
Ikabidi niwe mpole.
 
Hakuna uhusiano. Hicho anachokisema huyo muuzaji aidha ametengeneza yeye kichwani au amewekewa kichwani na wala hakipo nje ya kichwa chake.

Kuhusu manunuzi ya nguo za mtarajiwa ni vyema manunuzi yafanyike mara mgeni anapowadia, kama ni issue ya fedha ni vyema kuweka hiyo pesa mpaka muda utakapowadia. Ila maandalizi ya khanga na vitenge viwili vitatu ni lazima ila pale siku zinapokuwa jirani.
Mama zetu hasa kwenye mambo ya uzazi ukiona anakuonya juu ya suala fulani, hata kama ukiangalia unaona halina uhusiano, unatakiwa usilipuuzie wameona mengi.
 
Mkuu;
Naomba nikuambie hivi; Hakuna uhusiano wowote wa nguo/maembe na mtoto kuzaliwa na njano. Hakuna uhusiano kabisa. Ila, kwa kuwa sasa tiyari ushastukizwa, imani yako ikayumba, imani ya mkeo ikayumba, achana kabisa na chochote cha njano. Usipo fanya hilo, nakuhakikishia hata mtoto angezaliwa mweusi ka mjaluo bado mkeo atatafuta njano hata kwenye maaviii ya mtoto. Epuka kabisa njano kwa manufaa ya mkeo na kijacho
 
Mama zetu hasa kwenye mambo ya uzazi ukiona anakuonya juu ya suala fulani, hata kama ukiangalia unaona halina uhusiano, unatakiwa usilipuuzie wameona mengi.

Cha msingi hapo ni malezo juu ya uhusiano wa mambo hayo mawili.
 
Back
Top Bottom