Mkuu Jerrymsigwa, pole sana kwako na kwa mama mtoto na mtoto pia kwa hali hiyo. Binafsi ilinikuta na nilikuwa na umia sana, sasa hapo kuna jambo moja tu huwa ndiyo tatizo, mtoto atakuwa anasumbuliwa na gesi za tumboni, yaweza kuwa mama haweki chuchu yake vizur mdomoni mwa mtoto wakati wa kunyonya hivyo anakuwa na gesi tumboni, pia kila akimaliza kunyonya ajitahidi kuhakikisha mtoto anabeua kwa kumbeba wima akimuweka begani mwake mara baada ya kunyonya, amrushe rushe kidogo ili kutoa gesi tumboni, yaani hilo ndiyo tatizo kuu. Ukiwa mtu imani haba waweza fikiri mtoto kalogwa, lakini si hivyo.jaribu hii halafu nipe mrejesho hapa.