Mtoto mdogo kutoota nywele

Mtoto mdogo kutoota nywele

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
768
Ndugu

Kuna kakijana kangu kana miezi 7 sasa, aliwahi kunyolewa mara moja tu tangu amezaliwa akiwa na kama mwezi mmoja baada ya apo ukuaji wa nywele umekua wa kusuasua sana.

Kwa sasa zimeota ila sio za kutosha na sio nyingi na hazijaota kisogoni na nyuma karibu na shingoni, naomba msaada je, hili ni tatizo au ni kawaida?

Mtoto haumwi yupo sawa, MziziMkavu saidia.
 
Zitaota usijali…Kisogoni kutokuwa na nywele ni kawaida kwa watoto wengi na wengine unakuta hata upande mmoja hana nywele kwasababu ni upande mtoto anaolalia na mtoto analala sana...wangu mimi alikuwa hana nywele utosini mpaka akiwa na miaka 2 ndo mashahari yakaja kwa spidi...
 
okeee..
 
zitaota tuu wangu mi walikaa miezi 6 sasa wananywele tuu, vumilia dogo anaminywele na siyo nywele
 
Ndugu

kuna kakijana kangu kana miezi 7 sasa...aliwahi kunyolewa mara moja tu tangu amezaliwa akiwa na kama mwezi mmoja baada ya apo ukuaji wa nywele umekua wa kusuasua sana....kwa sasa zimeota ila sio za kutosha na sio nyingi na hazijaota kisogoni na nyuma karibu na shingoni...naomba msaada je hili ni tatizo au ni kawaida?mtoto haumwi yupo sawwa.. MziziMkavu saidia.
Usiwe na wasiwasi kadri atakavyokuwa na ndipo zitakapoota sio matatizo hayo ni kawaida tu.
 
Back
Top Bottom