Nyerere alitoa matibabu bure kwa watanzania miliono 25, alitoa elimu bure kwa wote waliotaka bila upendeleo, kulikuwa na ajira za kutosha kuanzia asie na elimu hadi mwenye elimu ya juu, wanaume waliokuwa wanawaonea wanawake walishitakiwa kwa mjumbe wa nyumba kumi au ofisi ya ccm. Nyerere alipigania uhuru wa Afrika kwa maslahi ya wanawake na watoto ambao walikuwa wanateseka zaidi.
Nyerere alikubali kuingia gharama kubwa kumtoa IDDI AMINI ambaye alivamia inchi yete na askari wake na kuwabaki wanawake wa Kitanzania. Mwanamke wa sasa ana dhiki kuliko wakati wa Nyerere. Kila kitu kipo lakini hawezi kununua. wakati wa Nyerere vitu vilikuwa vichache lakini alikuwa anauwezo wa kununua. Wanawake wa mijini wanahangaika mchana kutwa kupanga mbogamboga barabarani ili waweze kupata kipato cha kujikimu, wale wa vijijini ndiyo dhiki kabisa.
WANAWAKE PAMOJA NA MAMA YANGU ALIYEZAA WATOTO 12 NA KUWALEA BILA MFANYAKAZI WA NDANI NAWAOMBEA KWA MUNGU AWAJALIE UNAFUU WA MAISHA.