Mtoto mwenye kasi zaidi Duniani akazaliwa

Mtoto mwenye kasi zaidi Duniani akazaliwa

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Kwenye riadha huko Duniani miaka ilee palipata kutokea Mwamba alieitwa Tim Montigomery raia wa Marekani.

Siku Moja Tim alikimbiza upepo huku akisindikizwa na makelele ya wapenzi watazamaji wa Mchezo huo wengi wao wakiwa wamarekani wenzie na kufanikiwa kuwa bingwa wa mita 100.

Wakati hayo yakijiri upande wa pili kwa akina Dada nako mrembo Marion Jones nae alifanikiwa kuubalasa upepo na kuwa bingwa wa mita 100.

Wawili hawa sasa wakafanikiwa kuwa Binadamu wenye kasi zaidi Duniani.

Lakini wakaenda mbali na kufanikiwa kufunga ndoa na kisha wakapata Mtoto.

Nakumbuka katika kipindi cha Michezo cha television ya CNN kilicho kuwa kikiongozwa na Mreno Pedro Pinto, katika kipengele cha Play of the Day aliweka Video mbili tofauti za wawili hao kila mmoja akiwa anachukua ubingwa kisha mwisho akamaliza kwa kusema Mtoto mwenye mbio zaidi Duniani amezaliwa.

IMG_3049.jpeg
 
Back
Top Bottom