mtoto na mama yake iko vipi?

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Posts
7,956
Reaction score
5,149
Nimepata swali nikaona si vibaya wana JF mkanisaidia.Nina jamaa yangu ana miaka 34.Siku moja huyu jamaa alikwenda kumtembelea dada yake anayeishi kama 50km toka kwake.Alipofika huko akakutana pia na mgeni mwingine mwanamke mwenye umri kama miaka 40 ambaye alikuwa ameachika na ana watoto watatu.Yule mwanamke alipomwona tu jamaa yangu akampenda ghafla na kumwomba dada awaunganishe,kweli dada aliwaunganisha na baada ya muda wakawa wanajivinjari kwa raha zao. Baada ya kama miezi mitatu ya kujirusha,mwanamke akamwambia jamaa kuwa wewe ni mzuri sana na uko safi idara zote hivyo naona sikutendei haki maana wewe hujaoa na mimi nimeachika.Naona haya mazuri yote unayonipa ni bora ayapate mwanangu,tafadhali nakuomba umuoe mwanangu kwa kuwa najua atakuwa amepata mume bora kwa maisha yake na mimi nitakuwa mama mkwe ila siku nami nikizidiwa unihudumie japo kwa siri.Mtoto mwenyewe wa kike kwa sasa ana miaka 19 na hajui chochote juu ya uhusiano wa mama yake,na ameshatambulishwa kwa mchumba na mama yake lakini jamaa bado yuko njia panda.Ananiuliza aoe mtoto au abaki na mama mtu maana na yeye kitoto amekipenda.
 
mmh,ishi uyaone.mama hana aibu,siku moja moja na yeye amegwe.inaonyesha huyo mama hataki tena kuolewa,ila anapenda apate mtu wa kumkuna kuna japo mara moja moja.Wazazi wengine wakoje jamani,una hiyari u share na mtoto wako.mmhh hii kali.hapo hakutokuwa na heshima tena,na hiyo siri ikitoka nje jee?
 
 
jamaa akioa binti tu ajue huyo maza hatasita kumsukumia huyo binti
kwa njemba nyingine ambayo inamkoleza kwa mapigo.

ushauri ye ajilie tu kuku na mayai bila kuoa
 
Kuoa binti ambaye mliwahi kuwa na uhusiano haramu (zinaa) na mama yake kabla. Ni jambo lenye kuchukiza sana katika jamii, ukiwa wewe ni binadam uliye kamilika, basi lazima utajisikia vibaya kufanya jambo kama ilo, fikiria kuwa jambo kama ilo afanye mama yako mzazi, kisha dada yako ndio anapewa mume wa jinsi hiyo, utajisikiaje?
 

Very good advise lakini mmh?mifano mingine ni bora kutoisoma!
 
i see hichi ni kizazi cha laana tunachoishi.................!
wtf is that......................!
hapo jamaa asioe hata mmoja....................!
mama hafai na katoto keshakua harammu kwa jamaa kugusa................!
 
Huyu jamaa aendelee nao kama naye ni shetani kama huyo mama.

Mwanamke huyo ni mpuuzi kupindukia. Ni nyoka, tena shetani mkubwa. Kama anamtaka jamaa amwache waendelee na mambo yao bila kumwingiza binti (innocent) ambaye hasitahili hiyo adhabu. Siku huyo binti akijua wote (huyo mama na basha yake) watajisikiaje?

Mambo mengine yanakera sana. Angenambia mimi siku hiyo hiyo ningempiga chini bila huruma. Hapo anachotaka ni kumwendesha huyo kijana kama gari bovu. Na laana sana huyo mama.
 


Mkuu taratibu ni ushauri tu,najua una hasira lkn chuna mtu ale kuku na mayai...si unajua tena two in one?
 
Mkuu taratibu ni ushauri tu,najua una hasira lkn chuna mtu ale kuku na mayai...si unajua tena two in one?

Unajua mtume alimweleza nini kijana aliyemuuliza kama kuzini ni sawa?

"Kama usivyopenda watu wamzini mama yako, basi na wewe usiwazini mama wa wenzio" (watalaamu watarekebisha lugh akam nimekosea maneno ila maana inakuwa ni hiyo hiyo).

Unapomwongelea mama huongelei mwanamke wa kawaida. Ni mtu anayeheshimika sana katika jamii kwani siyo kila mwenye jinsia ya kike amepata hiyo baraka ya kuitwa mama. Kwa hiyo hata mama anatakiwa kuitendea haki hiyo heshima anayopewa. Huyu wa hivi hafai kabisa kuitwa mama (she has abused the status of motherhood)... to me she is insane!!
 


Mkuu nimekusoma ,hapo kwenye red uko sahihi kabisa. lakini kwa upande wa huyo mama anaona ni vyema jamaa huyo akimuoa binti yake ili na mwanaye afaidi maisha yake yote .Na kwa upande wake anajiona kama vile amefanya jambo la busara kabisa,mimi nimeshindwa kumshauri ndugu yangu straight nikaomba anipe kama siku mbili hivi nami nitafute cha kumshauri na natanguliza shukran kwa wote mnaonipa majibu.
 
Huyo mama ana laana naona ndo maana aliachika hana adabu hata kidogo.
sijui watoto wake anawapa malezi gani
 
Huyo ni wa kutwangwa kotekote na kupigishwa vuvuzela, kisha unamwacha....!
 
Pumbavu zake kabisa...:angry::mad2::mad2::mad2:
 
sepa si mama wala mtoto ni mashetwani tu wote.
 
Utandawazi, no bounds at all na watu mishipa ya aibu walishakata zamani sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…