St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,956
- 5,149
Nimepata swali nikaona si vibaya wana JF mkanisaidia.Nina jamaa yangu ana miaka 34.Siku moja huyu jamaa alikwenda kumtembelea dada yake anayeishi kama 50km toka kwake.Alipofika huko akakutana pia na mgeni mwingine mwanamke mwenye umri kama miaka 40 ambaye alikuwa ameachika na ana watoto watatu.Yule mwanamke alipomwona tu jamaa yangu akampenda ghafla na kumwomba dada awaunganishe,kweli dada aliwaunganisha na baada ya muda wakawa wanajivinjari kwa raha zao. Baada ya kama miezi mitatu ya kujirusha,mwanamke akamwambia jamaa kuwa wewe ni mzuri sana na uko safi idara zote hivyo naona sikutendei haki maana wewe hujaoa na mimi nimeachika.Naona haya mazuri yote unayonipa ni bora ayapate mwanangu,tafadhali nakuomba umuoe mwanangu kwa kuwa najua atakuwa amepata mume bora kwa maisha yake na mimi nitakuwa mama mkwe ila siku nami nikizidiwa unihudumie japo kwa siri.Mtoto mwenyewe wa kike kwa sasa ana miaka 19 na hajui chochote juu ya uhusiano wa mama yake,na ameshatambulishwa kwa mchumba na mama yake lakini jamaa bado yuko njia panda.Ananiuliza aoe mtoto au abaki na mama mtu maana na yeye kitoto amekipenda.