Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Abba Marcus Mayanja, mtoto wa msanii maarufu wa muziki nchini Uganda, Jose Chameleone, kupitia ukurasa wake wa TikTok ameongea kwa hisia kubwa na mashabiki wa baba yake kuhusu changamoto za kiafya anazopitia baba yake kutokana na matumizi ya kupitiliza ya pombe (Addiction).
Katika ujumbe wake huo uliojaa hisia, Abba aliwataka wote wanaomjali Chameleone kuwajibika kwa kumpa msaada wa dhati ili kumsaidia kujinasua katika changamoto hizo.
“Hii ni kwa mashabiki na kila mtu anayefurahia muziki wa baba yangu. Hata kama humpendi, hata kama hukubaliani na mambo aliyowahi kufanya—hata mimi mwenyewe nakubali kwamba yeye ni binadamu mwenye mapungufu mengi. Lakini mwishowe, Mungu alituleta duniani kupendana,” alisema Abba
Abba alisisitiza umuhimu wa kushughulikia changamoto za Chameleone kwa huruma, akisema, “Huu si wito wa kuwakumbatia watu wanaopenda baba yangu aendelee kuwa mlevi. Ni wito wa msaada kwenu,tunahitaji kushirikiana kwa pamoja kumsaidia ikiwa aachane na hali hii.”
Soma Pia: Jose Chameleone: Hakuna msanii wa Tanzania na Kenya anayetufikia kwa Kuimba, wanabebwa na Mashabiki tu
Abba pia alikemea waandaaji wa Matamasha ambao wanaendelea kumualika Chameleone kutumbuiza licha ya hali yake mbaya ya kiafya.
“Ni jambo la kushangaza kuona watu wengine wakimuona binadamu anayefanya huku akiwa anapitia changamoto ya kiafya, lakini bado wanampa matamasha. Ni wazi kabisa kuwa baba yangu hana afya nzuri, lakini waandaaji hawa wanaendelea kumualika na kumtumia kama chombo cha kuzalisha pesa,” aliongeza Abba