KAKA NASOKI
Senior Member
- May 25, 2016
- 191
- 212
Dina (sio jina halisi) ni mama wa watoto 3 ambao wote kwa sasa wanafanya shughuli zao na wako vizuri.
Wakati anaolewa alimkuta mumewe na watoto wawili. Katika malezi aliwalea wote kwa usawa bila kubagua na watoto wakawa wanapendana sana, igawa wote kwa sasa ni watu wazima wanajitegemea lakini hawakuacha kupendana. Siku moja akaja binti wa miaka 21 kwa Dina , wakati huo mumewe alisha fariki yapata mwaka mmoja uliopita. Alipofika ofisini kwake (Dina ni mjasiriamali) alishangaa kumuona binti anafanana sana na binti wake wa mwisho aitwae Eggy (sio jina halisi), binti akauliza hapa ndio ofisi ya mama aitwae Dina? akamjibu ndio.
Akamwambia mimi naitwa Leah (sio jina halisi), nilkuwa namtafuta baba yangu mzazi anaitwa Mike (sio jina halisi) akamwambia kweli huyo alikuwa mume wangu lakini kwa sasa ni marehemu. Binti akamwambia mimi ni mtoto wa Joyce (sio jina halisi) ameniambia baba yangu anakaaa Dar - Mikocheni. Dina akakumbuka huyo Joyce alikuwaga binti wao wa kazi na aliondoka ghafla siku moja kurudi kwao. Mama akaunganisha dots akajua kilichotokea, basi akamwambia ngoja nikuitie ndugu zako wengine uwafahamu.
Akawaita watoto wake waje pale ofisini kwake Upanga, watoto wakaja kufika tu wakamwambia mama yao, mbona huyu anafanana na mdogo wetu Eggy? akawajibu huyu ni mdogo wenu anaitwa Leah niwmewaita mfahamiane. Dina akamuuliza leah enhe! uanakaa wapi na unataka tukusaidieje?
Kama kukaa unweza kaa kwangu utafute kozi yoyote nikulipie, Leah akasema kwa sasa nakaa Mwananyamala kwa mama mkubwa, ila sipapendi kwani anauza pombe za kienyeji, ningependa kupanga chumba changu mwenyewe, nifanye biashara na sio kusoma. Basi kaka mkubwa akamuuliza kupanga mwaka mmoja shilingi ngapi?
Akasema laki 9 akampa palepale na Dina akamwambia furniture atachukua za marehemu babayako kwani ziko stoo hakuna anayetumia, kaka yake mwingine akampa laki 7 akasema kaanze biashara. Ikawa Leah anendelea na maisha yake binafsi lakini hakuacha kwasiliana na Dina pamoja na kaka zake na alikuwa akiwatembelea mara kwa mara majumbani mwao na kwenye bashara zao. Siku moja Leah akampigia Dina simu kumtaarifu ana mimba, Dina akamwambia njoo ujifungulie hapa nyumbani, akamwambia mama mkubwa amesemma nikajifungulie kijijini. Baada yakitambo kidogo Leah akampigia simu mama (Dina) kumtaarifu kajifungua ila mtoto amefariki. Maisha yakaendelea, Eggy mtoto wa Dina akawa anaolewa akamjulisha Leah akamuuliza tarehe, siku ya send off ilipofika Leah akaja nyumbani amabako sherehe ilipangwa kufanyika hapo kwenye bustani ya nyumbani, kufika akakuta pamepambwa, akauliza mbona hamkuchukua viti vya gold? mama akamjibu hivyo bei yake iko juu ingeharibu bajeti yetu Leah akasema vinapatikana wapi?
Akamtajia Leah akaenda akaleta viti 500, Dina hakutegemea msaada huo, yeye alimjulisha tu habari ya kuolewa Eggyna hakutegea mchango toka kwake, pia alishangaa kuona gari alilokuja nalo akiendesha mwenyewe.
Sherehe ikapita maisha yakaendelea (ili kujua zaidi soma Part 2)