MwanaNaomba kuondolewa ujinga, nimeulizwa na mtoto mdogo anayesoma darasa la tatu nimeshindwa kumjibu na kuishia kumpigia stori nyingine ili asahau swali lake, lakini kamekomaa kila muda kananikumbusha.....sijui nani amekatuma!! Msaada tafadhali...
nakubaliana na wewe.AhsanteMtoto wa kike kiswahili ni msichana. Mtoto wa kiume ni mvulana.
Wakipita umri wa utoto wote ni wana.
Ukitaka kuwatambulisha kwa nasaba ya uzazi mtoto wa kiume ni bini na wa kike ni binti.
HahahahMtoto wa kiume anaitwa Barobaro
Naunga mkono hoja. NdiyooooooooKatavi chukuwa ili jibu
Tukubaliane kuwa kiswahili kimetohoa maneno mengi toka kiarabu. Tunadai siku zote kuwa kiswahili ni kibantu lakini bado kuna ule uarabu ndani ambao utatufanya baadaye kiswahili kiitwe kreori sababu maneno mengi tumetohoa. Basi tungechukua kwenye makabila yetu sema kuwa msichana utamuita kigori wangu na mvulana utamuita morani wangu au kabila lolote otherwise tukubali tulishakubali kamusi ya kiswahili ambayo imeandaliwa na watu wa pwani ndo official tusipinge. Juma bin Kiute au Jamila binti mafuta.Bin au Ibn na Bint ni maneno yanayotokana na lugha ya Kiarabu, mnatakiwa kuwa makini na jinsi mnavyotaka kuyatumia.
Sawa sawa kabisa , niongezee kidogoTukubali ukweli kwamba mtoto wa kiume ni mvulana na wa kike ni msichana.lakini unapotaka kuwatambulisha kwa nasaba iwe mtu mzima wa jinsi a ya kike au kiume ndo maneno binti au bin yanapotumika.. mwana=mtoto wa fulani