Mtoto wa kike huitwa "BINTI" wa kiume anaitwaje?

Mtoto wa kike huitwa "BINTI" wa kiume anaitwaje?

Mwanzisha mada naomba niendeleze kidogo kwa kutoka nje ya mada

Kijana na binti wasioolewa lakini 'wakatenda' lugha inayotumika ni Kijana kamdunga mimba binti

Kumdunga ni neno linaloonyesha kisichotrajiwa kwa maana ya kuwa ni nje ya utaratibu

John(mwanaume) katika maana tuliyoeleza akichepuka na Farida(Mwanamke) wote katika ndoa au mmoja akiwa ndani ya ndoa, kinachotokea ni John Kampachika Farida Mimba

Kumpachika ina maana ya 'pachika' shikiza tu lakini siyo halisi (original) zao la uchepuko

Kihaule na Mkewe Chausiku katika ndoa,siyo stara kumtaja mwanaume katika uja uzito. Kumbuka si mimba ni uja uzito. Kwa mfano, Chausiku ana uja uzito! inatosha

Ukisema Chausiku ana uja uzito wa Kihaule utakuwa umetukana kwasababu hawa ni wana ndoa hutakiwa kuweka doubt!

Ukisema hivyo unathibitisha kuwa ujauzito wa Chausiku ni wa Kihaule.

Si kazi yako kuthibitisha ujauzito katika ndoa, unachoweza kufanya ni kuzungumzia Ujauzito wa Chausiku tu kwamba ni mjamzito

Ni makosa pia kusema Chausiku amebeba mimba.
Mwanamke aliyepata mimba tu ndiye anabeba, Chausiku habebi ana mume hivyo ana ujauzito

Kwasisi wa Pwani masuala ya ujauzito yanaelezwa kikeni zaidi kwa mwanaume ni 'silent' kidogo. Kwa mfano Binti Sudi ni Mjamzito ikimaanisha binti wa mzee Sudi ni mjamzito
Ukiulizwa yupi? Kwa maana wapo mabinti wengi utasema mkewe Makame Usi

Hata hivyo ukisogea kule Musoma, Nyakato au Geita ni rahisi sana kusikia Malima kamtia mkewe Mimba! lah!
 
Naomba kuondolewa ujinga, nimeulizwa na mtoto mdogo anayesoma darasa la tatu nimeshindwa kumjibu na kuishia kumpigia stori nyingine ili asahau swali lake, lakini kamekomaa kila muda kananikumbusha.....sijui nani amekatuma!! Msaada tafadhali...

Binti Ni mtoto wa kike
Mwana Ni mtoto wa kiume

bin Ni neno la Kiarabu linaloanzia Mwana Katika Kiswahili.
Bin Adamu maana yake Mwana wa Adam au Mwanadamu.
 
Kwa uelewa wangu hilo neno bin ni kwa kiswahili fasaha ni wa. Unaweza kuniiita JUMA bin Abdalah manaye ni JUMA wa Abdalah. Mana ya neno bin ni wa .inaonyesha huyu anamilikiwa na nani.ni kama binadamu mana yake ni wa ADAMU kiuhalisia. Mana yake Sisi ni wa ADAMU.Bin ADAMU = wa ADAMU.

Kwa kimasai ndio unaposikia Daniel ole Njoolay.ole ni wa . ila sio jina halisi ni kuonyesha kuwa daniel ni Wa njoolay.Christopher ole sendekeka. Yaani huyo Christopher ni wa Sendeka. Hata MTU akikuuliza huyu mtoto ni Wa nani utamjibu ni wa CHACHA . bin ni kiarabu likimaanisha wa. Hiyo inatumika kwa jinsia zote. Mfano kwa lugha ya kikurya ole/bin inatamkwa o pekee.mfano. MARWA o Mwita. Mana yake MARWA wa Mwita. Kwa kiarabu tungetamka MARWA bin Mwita na kwa kimasai tungetamka MARWA ole MWITA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanzisha mada naomba niendeleze kidogo kwa kutoka nje ya mada

Kijana na binti wasioolewa lakini 'wakatenda' lugha inayotumika ni Kijana kamdunga mimba binti

Kumdunga ni neno linaloonyesha kisichotrajiwa kwa maana ya kuwa ni nje ya utaratibu

John(mwanaume) katika maana tuliyoeleza akichepuka na Farida(Mwanamke) wote katika ndoa au mmoja akiwa ndani ya ndoa, kinachotokea ni John Kampachika Farida Mimba

Kumpachika ina maana ya 'pachika' shikiza tu lakini siyo halisi (original) zao la uchepuko

Kihaule na Mkewe Chausiku katika ndoa,siyo stara kumtaja mwanaume katika uja uzito. Kumbuka si mimba ni uja uzito. Kwa mfano, Chausiku ana uja uzito! inatosha

Ukisema Chausiku ana uja uzito wa Kihaule utakuwa umetukana kwasababu hawa ni wana ndoa hutakiwa kuweka doubt!

Ukisema hivyo unathibitisha kuwa ujauzito wa Chausiku ni wa Kihaule.

Si kazi yako kuthibitisha ujauzito katika ndoa, unachoweza kufanya ni kuzungumzia Ujauzito wa Chausiku tu kwamba ni mjamzito

Ni makosa pia kusema Chausiku amebeba mimba.
Mwanamke aliyepata mimba tu ndiye anabeba, Chausiku habebi ana mume hivyo ana ujauzito

Kwasisi wa Pwani masuala ya ujauzito yanaelezwa kikeni zaidi kwa mwanaume ni 'silent' kidogo. Kwa mfano Binti Sudi ni Mjamzito ikimaanisha binti wa mzee Sudi ni mjamzito
Ukiulizwa yupi? Kwa maana wapo mabinti wengi utasema mkewe Makame Usi

Hata hivyo ukisogea kule Musoma, Nyakato au Geita ni rahisi sana kusikia Malima kamtia mkewe Mimba! lah!
Duh......Asante Nguruvi3 kwa kuniongezea uelewa.
 
Sawa sawa kabisa , niongezee kidogo
Bin ni kiunganishi cha uzawa wa mwanaume kwa maana ya Juma Bin Hussein ikimaanisha Juma aliyezaliwa na Hussein. Asaha binti Maftaha kwa maana hiyo hiyo lakini kikeni

Mtoto anazaliwa kama mtoto wa kiume kwa maana yake na wa kike vivyo hivyo
Wanapoelekea umri wa balegheh au kuvunja ungo wanaitwa Wavulana au Wasichana

Katika umri wa balegheh na ungo huitwa Kijana na Binti
Ndiyo maana utasikia Kijana wa Katavi kamdunga mimba binti Mbonde

Baada ya umri wa kuzaa hadhi zao hubadilika na kuwa mwanaume na Mwanamke
Utasikia mwamaume huyu mkware au mwanamke yule mwingi, ushamfaham eeh

Ukienda Ushirombo au Machame kidogo utatatizika. Unaweza kusikia 'kuna mwanamke kapita hapa amebebe mwanaume' kwa maana ya mwanamke kabeba mtoto wa kiume
Kule hakuna category ni mwanaume na mwanamke! period
shukranimaneno haya kwa lugha zetu yapo.km wahaya.utofautisha mtototo wa kike na wa kiume kwa majina "mwiski(msichana),msigazi(mvulana).mwala wa(binti wa) mtabani wa bin wa).mushaija(mwanaume),mukazi(mwanamke).nawaomba BAKITA watusaidie kutupa maneno sanifu kama wanatusoma.
 
Back
Top Bottom