ASANTE KWA MTOA HII THREAD, IMEKAA KIUTU UZIMA PIA IMEELIMISHA SANA HASA KWA MTU MZIMA ANAYEJUA/THAMINI MAANA, HAKI,MALEZI,UMUHIMU,FAIDA,HASARA,MAJUKUMU,YA FAMILIA NA WATOTO WETU.
KUMBUKA KUNA TABIA ZA KURITHI, SO UKITAKA KUWA NA WATOTO WENYE MAMA/BABA TOFAUTI BASI OMBA MUNGU SANA HAO WAZAZI WAO WAWE WENYE TABIA NZURI NYINGI NA MBAYA KIDOGO , LAKIN UKIPATA MZAZI MWENYE TABIA MBAYA NYINGI NA NZURI KIDOGO, HAPO TENA UTAKUWA UMEWASHA MOTO KWENYE FAMILIA HATA UKAJUTA KWA NINI UMECHANGANYA TABIA KWENYE FAMILIA MOJA.
NINA MFANO 1 HAI.
Kuna ndugu yangu ana watoto wa kiume, alikuwa na shida sana na mtoto wa kike japo yeye ndoa yake inaendelea kuwepo, akatafuta huko mwanamke akamzalisha bila kufuatilia sana tabia ya yule mwanamke wa nje(kumbe anatabia mbaya kupita maelezo). Baada ya mwanamke kujifungua, Mwanaume akampa taarifa mkewe alikasirika sana lakin baadaye wakasuluhisha na maisha yanaendelea,mke alimwambia akifika 3 years amlete home,mtoto akaletwa analelewa vizuri sana na mtoto anaheshima nzuri sana kwa Mama yake mlezi,baba na kaka zake , ana 20yrs huwezi kujua kama ni mama tofauti kwa jinsi wanavyoishi kwa upendo. SIJUI NI UJINGA UNAMSUMBUA HUYU MWANAUME SIELEWI, kwani Mwanaume akazaa tena na mwanamke yuleyule wa nje mtoto tena wa pili, naye pia akaletwa pale home na kulelewa na mkewe tena LAKIN cha ajabu huyu mtoto ni tofauti kabisaaa kitabia na hawa watoto wengine tabia yake ni mbaya sana sana kwa kila mmoja ktk hiyo familia hata dada yake hampendi kabisa. BABA yake anatamka kuwa anajuta knn alirudia tena kuzaa na yule mwanamke,,ila sasa imejulikana kuwa kumbe huyu mdogo karithi tabia nyingi toka kwa Mama yake, wakati yule mkubwa karithi toka kwa Baba ndiyo maana hakuleta shida ktk malezi pamoja na kuelewana na nduguze.Mama mlezi,baba,watoto wote wanaendeshwa na huyu mtoto kupita maelezo kila wanalomfanyia hakubali,haelewi,hasikii wamempeleka kwa mwanasaikolojia wala haisaidia,wapo tu wanasubiri muujiza wa MUNGU utokee abadilike tabia.
Kupitia huu mfano naamini utaongezea ufahamu zaidi ,juu ya ule uliopewa na wana JF wengine.