Baada ya hii so touchy thread hatimaye Mjukuu Mtiifu napanda kitandani nikitabasamu kwa kicheko............Klorokwini!! I cant you Mkuu, you are another loh........eti watakuloga enitaim
...kaunga acha tu,
Kuna mdada mwenye matatizo ya uzazi aliwahi kuniambia hataki wazo la ku adopt.
Yu tayari kuuza kila kilicho chake agharamie matibabu abebe mwenyewe Mimba yake.
Mdada kama huyo, (pamoja na maombi na kuelimishwa risks za infant/maternal mortality)
ni nadra sana kwa uliye na mtoto/watoto kumuelewa kilio chake.
Hivyo ndivyo ilivyo kwangu.
Ninavyotamani kuwa na Binti wangu mwenyewe, yataka imani thabiti kukubaliana na usemi shukuru ulichojaaliwa.
Najua Mw'Mungu anakijua kilio cha rohoni mwangu. Nilimtanguliza, na bado naendelea kumtanguliza.
Ila mnh, muda wa ku enjoy na "princess" unanitupa mkono,...
Mbu hapa umenisikitisha mwenzio asubuhi asubuhi lol!
Mwe Maty we acha tu.....mie jana kaniliza na kunifanya nimuote !!!
...kuna wa manjano na matende, shaurilo!
Hivi, kwani kuoa/kuolewa ndio kuzaa?
Msipojaaliwa mtoto je?
Kama hayo ni kweli, mpe huyo mkeo space na umwambie bado unamhitaji maishani. Utakuwa uamuzi bora kuliko wa kutafuta mwanamke mwingine ili uzae nae. This is risky, unaweza ruka jivu ukakanyaga moto.
Pia huna uhakika kama mwanamke utayempata akakuzalia mtoto wa kike, anayedetermine jinsi ya mtoto ni mwanaume.
Mwe Maty we acha tu.....mie jana kaniliza na kunifanya nimuote !!!
ASANTE KWA MTOA HII THREAD, IMEKAA KIUTU UZIMA PIA IMEELIMISHA SANA HASA KWA MTU MZIMA ANAYEJUA/THAMINI MAANA, HAKI,MALEZI,UMUHIMU,FAIDA,HASARA,MAJUKUMU,YA FAMILIA NA WATOTO WETU.
KUMBUKA KUNA TABIA ZA KURITHI, SO UKITAKA KUWA NA WATOTO WENYE MAMA/BABA TOFAUTI BASI OMBA MUNGU SANA HAO WAZAZI WAO WAWE WENYE TABIA NZURI NYINGI NA MBAYA KIDOGO , LAKIN UKIPATA MZAZI MWENYE TABIA MBAYA NYINGI NA NZURI KIDOGO, HAPO TENA UTAKUWA UMEWASHA MOTO KWENYE FAMILIA HATA UKAJUTA KWA NINI UMECHANGANYA TABIA KWENYE FAMILIA MOJA.
NINA MFANO 1 HAI.
Kuna ndugu yangu ana watoto wa kiume, alikuwa na shida sana na mtoto wa kike japo yeye ndoa yake inaendelea kuwepo, akatafuta huko mwanamke akamzalisha bila kufuatilia sana tabia ya yule mwanamke wa nje(kumbe anatabia mbaya kupita maelezo). Baada ya mwanamke kujifungua, Mwanaume akampa taarifa mkewe alikasirika sana lakin baadaye wakasuluhisha na maisha yanaendelea,mke alimwambia akifika 3 years amlete home,mtoto akaletwa analelewa vizuri sana na mtoto anaheshima nzuri sana kwa Mama yake mlezi,baba na kaka zake , ana 20yrs huwezi kujua kama ni mama tofauti kwa jinsi wanavyoishi kwa upendo. SIJUI NI UJINGA UNAMSUMBUA HUYU MWANAUME SIELEWI, kwani Mwanaume akazaa tena na mwanamke yuleyule wa nje mtoto tena wa pili, naye pia akaletwa pale home na kulelewa na mkewe tena LAKIN cha ajabu huyu mtoto ni tofauti kabisaaa kitabia na hawa watoto wengine tabia yake ni mbaya sana sana kwa kila mmoja ktk hiyo familia hata dada yake hampendi kabisa. BABA yake anatamka kuwa anajuta knn alirudia tena kuzaa na yule mwanamke,,ila sasa imejulikana kuwa kumbe huyu mdogo karithi tabia nyingi toka kwa Mama yake, wakati yule mkubwa karithi toka kwa Baba ndiyo maana hakuleta shida ktk malezi pamoja na kuelewana na nduguze.Mama mlezi,baba,watoto wote wanaendeshwa na huyu mtoto kupita maelezo kila wanalomfanyia hakubali,haelewi,hasikii wamempeleka kwa mwanasaikolojia wala haisaidia,wapo tu wanasubiri muujiza wa MUNGU utokee abadilike tabia.
Kupitia huu mfano naamini utaongezea ufahamu zaidi ,juu ya ule uliopewa na wana JF wengine.
naomba kujua mcmamo wako hapo utakapopata wa kiume, nae utamchukua?..2 b honest Mbu kuna ugumu sana kwa mwanamke kukubali hii ishu, tena kwa "binti" khaa...kingine ni kwamba utataka kumchukua huyo binti akiwa na umri gani?
Mhhh..hapo pagumu...
lakini hasara mojawapo ni kwa huyo mtoto atakayezaliwa, kukosa upendo wa wazazi wote wawili, tatizo ambalo linaweza kumuathiri mtoto psychologically. Kama alivyosema mjumbe mmoja hapo juu, kama kuna uwezekano wa kusameheana na ex-wife wako, itakuwa ni njema sana, ili muweze kulea watoto wenu kwa pamoja. Hakuna aliye perfect katika dunia ya leo!
Ni mawazo yangu tu......
duh mawazo mengine bana?????????
ila nakupongeza kwa kuwa na hamu ya kuwa na mtoto wa kike !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! sema hizo mikakati sizikubali
Nenda shule kasome biology. Unafikiri mke mwingine ndo atakuzalia wakike? Kweli we wa zamani.
...kuna nyakati hunijia wazo nitafute mw'mke anizalie mtoto wa kike, aniachie mtoto (aendelee na maisha yake.) Sihitaji mke:nono:, wala kujaribu mtoto mwingine na my Ex-Wife wangu, (mama wa wanangu wawili wa kiume.)
Nini faida/hasara za jambo hilo?
...mnh?, lile wazo langu la kutafuta mke JF nalisitisha kwanza, LOL!
...Nnunu, ahsante sana kwa mchango wako. Hilo la tabia wengi wetu tunali overlook pia, shukran sana kulitanabahisha kwa kina.
...Dada'ngu Nyamayao, kwa ufupi...nimeghairi wazo hili baada ya kupata maoni ya kutosha jana.
I will go for the 2nd Option...(Mke), then tutapojaaliwa mtoto, yeyote ...Awe wa kike/kiume/ mapacha haya.
...Dada'ngu Nyamayao, kwa ufupi...nimeghairi wazo hili baada ya kupata maoni ya kutosha jana.
I will go for the 2nd Option...(Mke), then tutapojaaliwa mtoto, yeyote ...Awe wa kike/kiume/ mapacha haya.