Mtoto wa Kikwete ashinda kwa kishindo

Nini maana yake?
Soma hapa chini...

 
Hivi Dogo Khalfani atakuwa akilipwa kiasi gani kwa kuwa Chipukizi Mkuu?

Mchungaji.Kishoka

Huu nao ni Ufisadi?

Hapa Kanisani kwetu Kyela kuna Mzee Mchungaji juu ,Kamati zote za maana zinaongozwa na Mama Mchungaji,kiongozi wa kwaya ni Mtoto wa Mchungaji,Sunday School kabinti ka mchungaji ,hii ndo Tanzania Mwanawane.
 
JK mwennyekiti,
Mama Salma (mke) mjumbe
Ridhiwani (mtoto) UVCCM
Khalfani (mtoto) mjumbe wa Baraza la Chipukizi na UVCCM

Sasa chama cha kifamilia na kikabila ni CHADEMA au CCM?

List ni ndefu zaidi..

Kawambwa plus nduguze na Jk wawili
 
JK mwennyekiti,
Mama Salma (mke) mjumbe
Ridhiwani (mtoto) UVCCM
Khalfani (mtoto) mjumbe wa Baraza la Chipukizi na UVCCM

Sasa chama cha kifamilia na kikabila ni CHADEMA au CCM?

Teh teh Mpwaaaaa hii ndio SIASA YA BONGO!

NO COMMENT

 

  • Kitaifa/kiserikali umri wa kuanza kupiga kura ni miaka 18. Hata hivyo hii aizui jumuiya za kichama kuwa na chaguzi zao za ndani kutokana na mfumo wake. Ama ni kwanini umri huo umewekwa natumai unajua fika maana yake, kwamba ndio umri uliofikiliwa kuwa ndio muafaka kwa kijana kuweza kuchagua viongozi wake kitaifa/kiserikali . Ni umri ambao unasadikika kuwa kijana anaweza kuanza kujitegemea na kuwa na maamuzi yake binafsi.

  • Kusafiri peke yao ama kusindikizwa inategemea na mahala wanapokwenda. Kwa kuwa mkutano huo ulifanyika mkoani Morogoro hapana shaka wajumbe wake toka mikoa mbalimbali, washiriki wake walisafiri kwa pamoja chini ya wasimamizi wawili ama mmoja na sio kwa kila chipukizi kupelekwa na mzazi wake. Hii ni jumuiya/kitengo cha chama hivyo kuna taratibu nzuri za kuwasafirisha wajumbe wake.

    Aidha gharama za usafiri, malazi na mahitaji mengine ya mkutano yanagharamiwa na chama, pamoja na waandaaji wake(kichama).

  • Kimsingi kuingia chipukizi ya CCM sio jambo la lazima. Hivyo sio haki kwa mzazi kumshurutisha mtoto wake kujiunga. Mtoto anaweza kupenda kuwa chipukizi kutokana na kupenda shughuli zake nae kutamani kujiunga nao. Mikutano mingi mikubwa ya Chama(CCM) hufunguliwa na gwaride la chipukizi, haraiki ya chipukizi na mambo kadha wa kadha ya watoto hao. Hii pekee inaweza kumvutia mtoto yoyote kujiunga pasipo ushawishi wa mzazi wake.

    Miaka ya chama kimoja hali ilikuwa tofauti kidogo, kwani ilikuwa ni suala la kitaifa zaidi kuliko la kichama.

  • Lengo kubwa sio kujenga itikadi ya kubaguana, zaidi ni kujenga umoja miongoni mwao, kujua kazi za chama chao pamoja na madhumuni yake. Vitu ambavyo vilikuwa vikifundishwa kwa watoto wote(shuleni) kabla ya kurudi kwa vyama vingi.

    Hata baadhi ya vyama vingine naona taratibu wanaanza kuwa na utaratibu kama huu. Nimeona baadhi ya vyama kwenye mikutano yao, viongozi wao wa kitaifa wakivishwa mashada na skafu na watoto(chipukizi). Sidhani kama huko wanafundishwa itikadi mbaya! Ingawa maneno ya viongozi na wafuasi wao yana kila dalili ya itikadi mbaya dhidi ya CCM.

Mengine unaweza kuyafahamu vizuri kwa kupitia nukuu hizi...


 
Watanzania sijui ni nani alituroga mpaka tukabadilika na kuanza "KUABUDU" Siasa namna hii...!!!
 
JK mwennyekiti,
Mama Salma (mke) mjumbe
Ridhiwani (mtoto) UVCCM
Khalfani (mtoto) mjumbe wa Baraza la Chipukizi na UVCCM

Sasa chama cha kifamilia na kikabila ni CHADEMA au CCM?
...Nimeipenda hii...
 
Please guys, let us give a kid a break!
Amegombea, watu wamempigia kura.. ndio utamu wa demokrasia!
Hail to The Great Thinker Nyani Ngabu bin Julius.. Miafrika ndivyo tulivyo!

Hebu anaglia hii ripoti ya Mwananchi..

" Mtoto wa Kikwete aula UVCCM"
By Samuel Msuya - Morogoro.

".......Wajumbe wa chipukizi wa nchini kote wakiongozwaa Makatibu wa Mkoa wa UVCCM walimchagua Halfani huku wengi wao wakiwa hawajawahi kumuona na hata kumsikia akiwaomba kura. Wagombea wengine waliokuwako walijieleza na kuomba kura, lakini wakaambulia patupu...."

Jee inamaana alichaguliwa in absentia?

 
Ingekuwa wameshinda kwa kishindo shule hata mimi ningewapongeza. Kweli hili inaonyesha tu jinsi our priorities zilivyokuwa warped!

Amandla....
 
Nchi hii atari sana,kwa nini baba yangu akuchagua siasa,kwani ata kama uwezo wako mdogo aijalishi utawaongoza tu,na kama kilaza lakini baba ndio hivyo kama JK ndio basi utapewa vyeo ambavyo ata majukumu yake uyajui.

Uwezo wa ridhiwani ni wakuungaunga sana sijui uyo mtoto,ata maksi zilikua za kudesa lakini ana vyeo ambavyo ata details zake afahamu.

SISI MACHO LAKINI IPO SIKU TUTACHOKA.
 
JK mwennyekiti,
Mama Salma (mke) mjumbe
Ridhiwani (mtoto) UVCCM
Khalfani (mtoto) mjumbe wa Baraza la Chipukizi na UVCCM

Sasa chama cha kifamilia na kikabila ni CHADEMA au CCM?

Ndugu yangu kamende ulikuwa hujui kuwa CCM wana siasa za kifamilia zaidi kuliko vyama vingine? ndani ya CCM kuna vimungu mtu vya kiukoo ndivyo vinavyoendesha chama havitaki familia zingine ziingie humo havionekani kwa sababu chama ni kikubwa ukoo mmoja uko toka ngazi ya mtaa, kijiji, wilayani, mkoani wizarani hadi Taifa utadhani wengine hawafai.
Watajifanya wanandaa chipukizi lakini wako mstari wa mbele kulaumu CHADEMA kuwa ni chama cha ukoo. Kwa kuanzia nitawaleteeni ukoo wa Kingunge muone picha halisi walio ndani ya chama hadi serikalini. Wanaposema CCM ina wenyewe usifiri propaganda tu za chama ni kweli wengine washika vibendera.
 
Hongereni Chipukizi wote mlioshinda na kupata nafasi ya kuwakilisha chipukizi wengine!
ZZZZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII,
kwani nyie sisiemu hamna watoto wengine hadi mnachagua watoto wa viongozi kina kikwete, kina makala, majina hayo hayo kila siku, aaarrrrgggghhh
 
yaleyale ya kina Omar Bongo, tusipoangalia hawa watu wataingiza ufalme! Nyerere, Mwinyi, Mkapa wangeweza fanya hivyo ila walijua kutenganisha uongozi na familia! sasa hako katoto kameshinda through merit au through father influence?
 
Kuna watu humu JF sitaki kuwataja kwa majina wapo mstari wa mbele kukikosoa CHADEMA kuwa ni cha ukoo lakini sasa wamekuja na gia eti CCM wao wana-groom tu hawoni kuwa hiyo pia ni sababu tosha ya ubinafsi ukoonaism wanataka wawe wao tuuuu jamani.
 

Jamani mbona tunakuwa wasahaulifu?

Vyama vyote vikuu vya siasa vina idara zao za vijana,na hii yote ni mipango kamambe ya kuzalisha viongozi wa baadae ambao watakua chachu ya kueneza itikadi za vyama husika.

John myika,ZZ,msafiri mtemelwa,kafulila,Danda etc ni mifano ya wanasiasa ambao wameanza ngazi za chini sana kwenye vyama vyao.

Ukiondoa udhaifu wa mtu binafsi pamoja na kipaji,kiongozi bora ni yule alieanza kupewa uongozi utotoni.msome huyu bwana mdogo http://en.wikipedia.org/wiki/David_Miliband#Early_life
 


........Ghafla, Pamekuwa kimya!
 
JK mwennyekiti,
Mama Salma (mke) mjumbe
Ridhiwani (mtoto) UVCCM
Khalfani (mtoto) mjumbe wa Baraza la Chipukizi na UVCCM

Sasa chama cha kifamilia na kikabila ni CHADEMA au CCM?
Hivi Miraji(mtoto) ni nani tenaa,aah nimekumbuka,huyu ni msela tuu!!
 
Sasa wewe ukienda usalama wa taifa na wizara ya mambo ya ndani si ndio utalia kabisa ni undugunaizeshen theory,we acha tuu,soma alama za nyakati chukua kilicho chako then take a new move!!
 
ZZZZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII,
kwani nyie sisiemu hamna watoto wengine hadi mnachagua watoto wa viongozi kina kikwete, kina makala, majina hayo hayo kila siku, aaarrrrgggghhh
Pilipili usio'ila inakuwashia nini?
 

Wakati wa watu kupata madaraka na nafasi za kuongoza kutokana na uwezo hizooooooooooo zinaondoka. Matabaka hayooooooooooooooo yanagawika. Tupende tusipende Mlalahoi, "GO TO HELL". Wakati wa kupata elimu, kupata madaraka kutokana na uwezo wako kiakili kwa kuanzia chini na kupanda kidogo kidogo kama walivyopanda wao hawa MAFISADI umekwisha. Only the elite group that will own everything and you and me will deserve nothing.

MAFISADI watazidi kukusanya kila kilichopo, watakalia kila nafasi na kumiliki kila kitu na kiburi chao kuongezeka.

MWENYEZI MUNGU AWALAANI KWA KUWAONGEZEA MARADHI YA KUENDELEA KUTOTOSHEKA KILA WANACHOKIPATA, AWAONGEZEE VIBURI NA JEURI, NA AWAONDOSHEE KABISA UFAHAMU WA KUELEWA MAKUSUDI YA KUUMBWA KWAO, WASIJUE LIPI BAYA/OVU NA LIPI ZURI/JEMA, WAO WACHANGANYE TUU ILI ISAFIKE NJIA YAO YA KUELEKEA MOTONI, NAJISI HAWA.

NA SISI MUNGU ATUJAALIE SHUJAA MIONGONI MWETU AMBAE SIKU MOJA ATAWASGHULIKIA VILIVYO MAFISADI WATAKAOBAKIA KUWEPO WAKATI HUO. ATUONDOSHEE NA AISAFISHE NCHI YEU NA NAJISI HII NA UVUNDO WA MAISHA YA MAFISADI HAWA. MAISHA YA MAFISADI HAWA NI BALAA KWA WANYONGE

LAANATULLAAHI ALAL MUFSIDIIN.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…