Mtoto wa kiume, msaada


Yaani uko so insecure na suala la wewe kuwa mwanamke kiasi kwamba mumeo akisema anatamani kuwa na mtoto wa kiume we akili yako itasikia kwamba anadharau wanawake. Kuna watu pia huwa wanatamani kupata mtoto wa kike. Jaribu kufungua hiyo minyororo ya kifikra uliyojifunga mama
 
Yaani I m so surprised kuwa wengi wa wanawake wanachangia hii mada kama vile kutamani kuwa na mtoto wa kiume ni kosa la jinai. This is so boring badilikeni wabeijing maana mtafika mahali sasa mtaanza kuchukia wanaume bure.................
 


Stahili yake kabisa huyo!

Tena namuongezea kama si watoto wa kike huyo mke wa kumzalia hao watoto angempatia wapi!

kwa nini watu mnakuwa majuha namna hii?
 

Sijaelewa, or, may be am missing something! Zimetajwa mali hapa, does it mean malengo ni kumtafuta wa kiume ili awe mrithi? Yale yale! Au angependa kuona mtoto wa kiume anazunguka zunguka ndani ya nyumba ili roho yake itulie? Comeon, rafiki, mbona mnataka kuturudisha tulikotoka? Kwa nini usiwape uezo hao watoto wa kike waje kuwa kama kile unachotaka wewe, in terms of capability? Don't tell me kuwa you guys still don't believe in watoto wa kike? Don't you believe kuwa wakipewa uezo /nafasi wanaweza?

Ok, well, labda sikuelewa mada, au ni kuwa huyo rafikio mali zimekuwa nyingi sana kwa hiyo anaona zitawaelemea hao watoto wake watatu, kwa hiyo anawaongezea msaada?

Unless, kama rafiki yako ameongezewa roho ya imani, kutoa msaada kwa watoto wasio na uezo, nitamsupport, otherwise...mmh..napata taabu kuinunua idea...
 
Dina huyu Kaitaba na Rafikiye wana mawazo mgando!

hata sijui kwa nini Mungu alimpa hao mabinti wazuri ; mtu kama huyu ilimfaa asipewe uzazi kabisa; haelewi nini maana yake; hebu siku mmoja aropoke kwa wanawe haya maneno watayachukuliaje?
 

My take, siyo suala la minyororo, I would have the same opinion hata kama mtoa mada angeangukia kwenye suala la kutafuta nyongeza ya mtoto wa kike...
 
Kama anataka kwa njia yeyote ile basi hata ya ku adopt ni better, maana huyo mama hataiwezekana tena na kwenda kuzaa nje ya ndoa haitakuwa vema, while makubaliano ya kufunga kizazi wote waliafiki. After all mtoto ni mtoto haijalishi kike au kiume.

Kuadopt, unafanyaje?
 
Kuadopt, unafanyaje?

nenda kwenye vituo vya kulelea yatima tena hapo Arusha kuna kituo kimoja cha masista kinalea watoto wazuri sana! Wasiliana na village of hope Dodoma pia. Nimemwomba mungu aniongezee kipato nami nije kum adopt mmmoja!

Unaomba kulea wale wasio na wazazi wapo wengi sana! Ama ukisikia watoto wameokotwa jitolee kuwatunza kama una hela waweza kuwapata hata wanne!
 
Binafsi naamini watoto wa kike wanaweza tena sana lakini wanaweza tu kubeba majukumu yao kama ambavyo wanaume wanaweza kubeba majukumu yao na si zaidi ya hapo
 
Dina huyu Kaitaba na Rafikiye wana mawazo mgando!

hata sijui kwa nini Mungu alimpa hao mabinti wazuri ; mtu kama huyu ilimfaa asipewe uzazi kabisa; haelewi nini maana yake; hebu siku mmoja aropoke kwa wanawe haya maneno watayachukuliaje?
Ndio maana hakuropoka kwa wanawe mkuu. Mi sidhani kama ni kosa kutamani mtoto wa kiume. Msimuhukumu huyu bwana bure sijaona mahali popote akisema kuwa hawapendi watoto wake wa kike after all ukiwa na nyumba moja ukatamani kuwa na nyingine sio kosa japokuwa kuna watu wengi tu hawana hata sehemu ya kulala.
 
Da womanizer!

Anapo relate suala za urithi wa mali zake nayeye kutokuwa na watoto wa kiume ni mawazo mgando!
 
1.rafiki yako nakushauri asitafute mtoto wa hiari(adapt).........ni hatari
2.asihangaike,haohao aliompa mungu wanatosha.awarithishe kila kitu hao.
3.anaweza kuweka masharti kuwa hizi mali ni zenu peke yenu siyo na waume zenu...kuna tatizo hapo?
4.ila kama anataka watoto wake waje wauwawe na huyo mtoto mgeni ili awanyan'ganye mali i'ts ok,aendelee.kusaka
5.wote wa kike au kiume wana uzito unaolingana,tena ingekuwa mimi ningechekelea kupata wakike zaidi.
 
3.anaweza kuweka masharti kuwa hizi mali ni zenu peke yenu siyo na waume zenu...kuna tatizo hapo?

Alaaaaaaaaaaa kumbeeeeeeeee???!!!!!!!!!!!!


Tall umenena! nahisi hili ndio tatizo kubwa la huyu rafikiye! NI MCHOYO!
 
Ashukuru ana hata hao watoto wa kike, angeweza kukosa kabisa.

Akienda nje na kupata watoto wa kike atafanyaje? Hivi kuwa na mtoto wa kiume ni lazima? Mbona the most powerful man by some account, Obama, hana mtoto wa kiume na wala hajasweat?

Now that I think of it, George W. Bush naye hakuwa na mtoto wa kiume, Bill Clinton hakuwa na mtoto wa kiume.

Huu mfumodume noma kweli.
 
Hiyo ni kwa sababu wewe ni tall na yeye ni yeye mkuu....usisahau kila mtu na mapenzi yake
 
Aliyekwambia hajasweat nani????? We unayajua yote yanayopita katika akili ya Obama??? After all ni nani aliyekwambia ni lazima upende kuwa kama alivyo Obama, Bush au Clinton. Kwa hapa mkuu sijaona hoja kabisa...
 
Anataka apate watoto wa kiume japo wawili kwa njia yoyote ile, iwe ya kuokota mtoto wa kiume, kuzaa na mtu yeyote mradi mtoto akizaliwa awe wa kiume au vyovyote vile.
Mimi ningependa kujua kwanini anataka mtoto wa kiume na asiridhike na hao watoto wa kike aliojaliwa na Mungu. Kama anatafuta mrithi kutokana na hizo mali zake basi amuombe Mungu amsamehe maana hajui alitendalo na wala asithubutu kumtafuta mtoto wa kiume kwasababu hiyo ya mrithi. Nina mifano mingi sana ya kumpa kwa wanaume waliojaribu kufanya jambo kama hilo walijuta na wanaendelea kujuta.

Ushauri wangu awalee watoto hao Mungu aliompa fullstop hayo mengine ni zinaa na kujilisha upepo chini ya jua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…