SoC02 Mtoto wa kiume

SoC02 Mtoto wa kiume

Stories of Change - 2022 Competition

HIBISCUS 80

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2020
Posts
1,058
Reaction score
1,218
Habari za usiku huu Wana Jamiiforums,

Leo nataka kuongelea malezi ya mtoto wa kiume kwani kuna mahali naona jamii ya Tanzania pamoja na Africa kwa ujumla imepotoka au imejisahau sana katika kumlea na kumuandaa mtoto wa kiume kuwa baba na kiongozi wa familia yake.

Mtoto wa kiume anatakiwa kulelewa katika malezi ambayo yatamuandaa kuwa baba na kiongozi wa familia anatakiwa kutambua majukumu yake
Kumekuwa na wimbi kubwa la kuona kuharibikiwa watoto wetu WA kiume.

Tumekuwa na watoto ambao hawatambui kabisa majukumu Yao kama wanaume na hii imesababisha kuwa wa na watoto wanaotafuta wanawake wwnye uwezo wa kifedha ili tu waweze kupata pesa kwa urahisi
Tumekuwa na wanaume ambao wanakumbana na changamoto kubwa sana ya nguvu za kiume
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wanaume wanaokimbia majukumu Yao ya malezi kwa watoto wao.

Kumekuwa na ongezeko kubwa Sana la wanaume wenye kupenda utajiri wa haraka bila kufanya kazi.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wanaume wavivu
Miaka ya nyuma katika jamii nyingi za kiafrika mtoto wa kiume akifika umri Fulani anaanza kufundishwa kazi, anafundishwa majukumu yake kama mwanaume.

Kuna baadhi ya jamii zilikuwa na utamaduni wa jando kwa watoto wa kiume na huko watoto wanafundishwa ukakamavu, uvumilivu,uwajibikaji na hata ulaji wa vyakula.

Miaka ya nyuma kulikuwa na wanaume wachache sana wenye vitambi, lakini siku hizi Hadi vijana wadogo kabisa wanavitambi, wanauzito ulioopita kiasi na hii inachangia kwa kiasi kikubwa sana ongezeko la wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume.

Ushauri wangu kwa jamii kuhusiana na malezi ya mtoto wa kiume.

Jamii inapaswa kutambua makosa yaliyofanyika na kuyarekebisha.

Kwa kuanzia familia zirudishe malezi na mafundisho kwa watoto kuhusiana na wajibu wao kama wanaume, familia pamoja na nyumba za ibada na shule lazima zianze kutengeneza upya mafundisho na majukumu kwa watoto wa kiume.

Familia lazima zianze kufundisha watoto ulaji wa chakula uliobora wimbi la obesiity kwa watoto wa kiume litafutiwe dawa kuanzia nyumbani wakati watoto ni wadogo , watoto wanaona chisi kuku, sausage,mayai ,ndiioi vyakula Bora lakini tunapasa kuanza kuwaelejeza kuachana na aina hyo ya chakula kuepukana na tatizo la low sperm count au upungufu wa nguvu za kiume
Familia zianze kufundisha watoto madhara ya unywaji wa pombe uliopitiliza na unywaji wa pombe Kali kupitia kiasi.familia pamoja na jamii kwa ujumla ifundishe uwajibikaji.

Familia zianze ku discourage kabisa habari za ushoga tangu watoto wakiwa wadogo hii itasaidia watoto kutoa taarifa mapema wanapofanyiwa ubakaji.

Kwa muda mrefu jamii imekuwa ikipiga kelele sana kutaka kumnyanyua mtoto wa kike lakini mtoto wa kiume amesahaulika kabisa kabisa hii imesababisha uharibifu mkubwa sana kwa watoto wa kiume,jamii inapaswa kurudi nyuma na kurekebisha ,wanaharakati ni wakati Sasa wa kupaza sauti kuhusu watoto wa kiume.

Watoto wetu wamekuwa wakikimbilia madawa makali yenye madhara kwa ajili ya kuongezea nguvu za kiume ambayo yatawaletea madhara kwa miaka ijayo, ni wakati wa kuongea wazi na watoto wetu
Ni wakati wa kuwafundisha kazi watoto wetu, ni wakati wa kuwafundisha watoto wetu kuwajibika na kubeba majukumu Yao na sio kuyakimbia.

Mlee mtoto katika njia impasayo nae hataiacha hata atakapokuwa mzee
Tukomboe kizazi hiki pia kwa kuwafundisha watoto wetu WA kike kusimama katika nafasi zao kama wasaidizi na kuacha nafasi ya uongozi wa familia mikononi mwa mwanaume.

Asanteni
 
Upvote 1
Back
Top Bottom