DOKEZO Mtoto wa Miaka 10 ameajiriwa kazi za nyumbani Kimara Stop Over, ananyanyaswa sana, Waziri Gwajima msaada wako unahitajika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Matatizo madogo kama haya ndio ayatolee taarifa Kwa waziri?. Hapo mtaani kwao hakuna mjumbe, serikali ya mtaa hakuna?. Mambo madogo kama haya yadhughurikiwe na waziri?.
Kwani Waziri amekataa kuyashughulikia?
 
Yes Ni ngumu sana kuongilia familia YA MTU mwingine..mtoa maada umefanya Jambo la maana

Inaumiza mama mwenye watoto kuendelea kunyanyasa watoto wenzake
Nina jirani yangu mmoja, ana mtoto wa kike wa miaka 6 au 7 hivi, sasa huyo mama anavyoongea na huyo mtoto wake, unaweza fikiri anaongea na mtu mzima mwenzake. Anamgombeza kwa sauti kubwa mno, kale katoto kamepoteza kabisa kujiamini.

Anamgombeza hata kwa mtoto kulia usingizini kwa kuota ndoto. Yaani usiku pametuliaaaa, unasikia tu mama ameanza kugombeza na kumpiga mtoto. Ni mwanae kabisa wa kumzaa, baba ni mkimya, sijui huwa anapotezea au anakosa cha kufanya. Huwa natamani hata nikamnyang'anye huyo mtoto, maana hakana raha kabisa kale katoto.
 
Duuh hawa mawaziri wakiona hv lazima wadate
 
Ujumbe UMEFIKA, kila mwenye mamlaka atawajibika katika nafasi yake.

Mtoa post, umetekeleza wajibu wako kama mwana jamii, MJUMBE wa mtaa AONE na awajibike, Maofisa wa USTAWI wawajibike, Polisi Kata awajibike.

Mwisho fundisho likipita kwa kiasi fulani watoto WATASALIMIKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…