Hapa mtaani kuna mama mmoja anaitwa Mama Nancy amemuajiri mtoto ambaye kwa umri sina uhakika lakini nahisi ana umri wa miaka 9 au 10, ameajiriwa kama house girl.
Kibaya zaidi Mama Nancy amekuwa akimnyanyasa huyo mtoto, anampiga anamfokea na inadaiwa amemkataza kuzungumza na watu wengine nje ya familia yake ili wasije wakamfungua akili.
Mtoto huyo amekuwa akiishi kinyonge muda mwingi, anapata mateso makali tena ya waziwazi ambayo sisi majirani tunaona, vipi kuhusu yale ambayo hatuyaoni yanayofanyika kwa ndani?
Mtaa unaoishi na ambao ndio mhusika huyo anapatikana unaitwa Umoja Street, ni Kimara Stop Over (Dar es Salaam).
Mtu ambaye anataka kushuhudia au kama Serikali inataka kufuatilia, wakifika hapo Stop Over, waulizie kwa Dereva Bodaboda kuwa wawapeleke Mtaa wa Dkt. Kayuni au Kanisa la Mabati.
Wakifika hapo nyumba hiyo ina geti la kijivu, chumba cha kwanza cha wapangaji, ndipo anaposhi mama huyo.
Mama huyo ni Mwalimu, anafundisha Shule ya Msingi ipo mitaa hiyohiyo ya Kimara.
Mtoto huyo ameajiriwa hapo wiki za hivi karibuni, ametokea nje ya Dar, aliyemleta ni mama mmoja (rafiki wa Mama Nancy) ambaye kazi yake anachukua Watoto wadogowadogo kama huyo house girl kisha anawabebesha bidhaa wauze mtaani, bidhaa kubwa anayowabebesha ni sabuni.
Mimi nazungumza kwa kuwa natarajia kuwa mzazi, hivyo ninapoona Mtoto mdogo kama huyo anafanyia hayo inamanisha nami Mtoto wangu ipo siku anaweza kufanyiwa kama hayo.
Mama Nancy ambaye ni mama wa Watoto wawili, anaonesha roho mbaya kiasi kwamba ni kama hana Watoto.
Naomba Waziri Gwajima kupitia Wizara yake amsaidie mtoto huyu pamoja na Watoto wengine wote wanaotolewa mkoani na rafiki wa mama Nancy kisha kuja mjini kutumikishwa.
Inawezekana wazazi wa Watoto hao ni masikini n ndio maana wanawaruhusu Watoto wao waje mjini bila kujua wanachopitia.