DOKEZO Mtoto wa Miaka 10 ameajiriwa kazi za nyumbani Kimara Stop Over, ananyanyaswa sana, Waziri Gwajima msaada wako unahitajika

DOKEZO Mtoto wa Miaka 10 ameajiriwa kazi za nyumbani Kimara Stop Over, ananyanyaswa sana, Waziri Gwajima msaada wako unahitajika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Maswala ya health and social care; naweza jiita mtaalamu.

Ni complicated issues kwa Tanzania sijamsikia mtu mwenye uelewa mpana na mwenye qualification sahihi kwenye sector ya afya kumzidi Dorothy Gwajima.

Ni hivi kwenye afya Dorothy Gwajima sio tu kwamba yeye mwenyewe ni medic she is also trained in management that includes finance aspects kama biashara ya afya, auditing and understands regulations za afya.

Tatizo la Dorothy Gwajima she is too girly tofauti na wataalamu wengi wa kike, lakini akisema akupigie health audit service ya papo kwa hapo (na kama Unaufahamu wa hayo mambo na namna huduma inavyokuwa regulated).

Niamini nikilwambia Dorothy Gwajima sio mzaha mzaha kwenye sector ya afya.

Hata huko services kwa standard za Tanzania hana mpinzani wa kumzidi: Iła kama nchi tunapwa.

Dorothy Gwajima is just too girly (anaweza kulia hovyo kwa mambo rahisi akawakera wengine) but trust me she is genius.

Katika wanawake waliłoko bungeni labda Ndalichako anaweza kuwa akili kubwa ambazo hawezi zisibitosha.

Vinginevyo Dorothy Gwajima kwenye kichambio chake anaweza kukuingizia concepts za quantum physics, WHO regulations na concepts za ā€˜International Standards of Auditing wakati anakukagua kama kilaza uwezi muelewa.

Dorothy Gwajima is something, her demeanour shouldn’t fool you; she is just girly but a very clever one.
Nipo na wewe bampa tu bampa.Nakuelewa sana.Huu unaoufanya ndiyo utu sasa.Unamueleza mtu kiuhalisi kwa manufaa mapana ya jamii.Bravo,Bravo & Braa!(mbili na nusu hizo ndugu balozi).
 
Hapa mtaani kuna mama mmoja anaitwa Mama Nancy amemuajiri mtoto ambaye kwa umri sina uhakika lakini nahisi ana umri wa miaka 9 au 10, ameajiriwa kama house girl.

Kibaya zaidi Mama Nancy amekuwa akimnyanyasa huyo mtoto, anampiga anamfokea na inadaiwa amemkataza kuzungumza na watu wengine nje ya familia yake ili wasije wakamfungua akili.

Mtoto huyo amekuwa akiishi kinyonge muda mwingi, anapata mateso makali tena ya waziwazi ambayo sisi majirani tunaona, vipi kuhusu yale ambayo hatuyaoni yanayofanyika kwa ndani?

Mtaa unaoishi na ambao ndio mhusika huyo anapatikana unaitwa Umoja Street, ni Kimara Stop Over (Dar es Salaam).

Mtu ambaye anataka kushuhudia au kama Serikali inataka kufuatilia, wakifika hapo Stop Over, waulizie kwa Dereva Bodaboda kuwa wawapeleke Mtaa wa Dkt. Kayuni au Kanisa la Mabati.

Wakifika hapo nyumba hiyo ina geti la kijivu, chumba cha kwanza cha wapangaji, ndipo anaposhi mama huyo.

Mama huyo ni Mwalimu, anafundisha Shule ya Msingi ipo mitaa hiyohiyo ya Kimara.

Mtoto huyo ameajiriwa hapo wiki za hivi karibuni, ametokea nje ya Dar, aliyemleta ni mama mmoja (rafiki wa Mama Nancy) ambaye kazi yake anachukua Watoto wadogowadogo kama huyo house girl kisha anawabebesha bidhaa wauze mtaani, bidhaa kubwa anayowabebesha ni sabuni.

Mimi nazungumza kwa kuwa natarajia kuwa mzazi, hivyo ninapoona Mtoto mdogo kama huyo anafanyia hayo inamanisha nami Mtoto wangu ipo siku anaweza kufanyiwa kama hayo.

Mama Nancy ambaye ni mama wa Watoto wawili, anaonesha roho mbaya kiasi kwamba ni kama hana Watoto.

Naomba Waziri Gwajima kupitia Wizara yake amsaidie mtoto huyu pamoja na Watoto wengine wote wanaotolewa mkoani na rafiki wa mama Nancy kisha kuja mjini kutumikishwa.

Inawezekana wazazi wa Watoto hao ni masikini n ndio maana wanawaruhusu Watoto wao waje mjini bila kujua wanachopitia.
Katie taarifa kwa mtendaji wa mtaa tu , litashughulikiwa haraka
 
Mkuu umefanya vizuri kutoa taarifa, nishauri tu jamii kuishi vizuri na hawa wasaidizi wa kazi. Najua hata humu wapo wenye kuwapa manyanyaso hawa ndugu zetu, tuwape haki zao za msingi na malezi pia .
 
Kwa taarifa yako nchi inahitaji watu wa aina ya Dkt Doroth. Kiongozi asiyechoka na mwenye unyenyekevu 24/7. Style zenu za uongozi wa kulindana za kijinga mkome
Kwani nimesema Dorothea hahitajiki?
Ninachosema ni kwanini msiwasiliane na viongozi waliopo huko mashinani na badala yake kila kitu mnamtegemea mtu mmoja kama wajinga?

Hapo karibu na Stop Over kuna Kituo cha Polisi pale Kimara Mwisho (Terminal) na hili nalo hamlioni?
 
Nipo na wewe bampa tu bampa.Nakuelewa sana.Huu unaoufanya ndiyo utu sasa.Unamueleza mtu kiuhalisi kwa manufaa mapana ya jamii.Bravo,Bravo & Braa!(mbili na nusu hizo ndugu balozi).
Naelezea uhalisia tu.

Shida ya Dorothy Gwajima ni too girly, halafu anatabia zinazofanana na wanawake wakawaida (tofauti na level zake za akili) hapo ndio watu wanashindwa kumuelewa.

Msikilize sasa akitoa kichambo kwenye sector ya afya. Utaona anaropoka if you are not technicsl on what she is on about., lakini kama unauelewa wa procedures za management za afya, and what she is mournin about and how eclectic she is ndio utaelewa uwezo wake.

Thamani ya kitu inatokana na value ya watu wanayoina, Iła kwa Dorothy Gwajima her African girlish demeanour shouldn’t fool you she is a genius.
 
aje tu kwangu apa mengine nitaleta mrejesho
Sasa,hebu turudi "Rau madukani"!Tujiulize.Huyo mtoto ni wa nani?Ametokea wapi?Kwa nini aajiriwe uyaya kwa umri huo?Hapo awali aliishije?Wapi na wapi?Halafu turudi sasa kwa mama Nancy.Kwa nini amemchukua awe yaya wake?Ni yaya kweli?Ni ndugu in yayas disguise?Hitimisho;Mama Nancy atamalizana na serikali "kiungwana".Vipi muendelezo wa mtoto/"yaya" kimaisha yake?
 
Naelezea uhalisia tu.

Shida ya Dorothy Gwajima ni too girly, halafu anatabia zinazofanana na wanawake wakaida.l (tofauti na level zake za akili) hapo ndio watu wanashindwa kumuwlewa.

Msikilize sasa akitoa kichambo kwenye sector ya afya. Utaona anaropoka if you are not technicsl on what she is on about., lakini kama unauelewa wa procedures za management za afya, what she is mousing about and how eclectic ndio utaelewa uwezo wake.

Thamani ya kitu inatokana na value watu wanayoina, Iła kwa Dorothy Gwajima her African girlish demeanour shouldn’t fool you she is a geniusz
Lakini,yeye ni mwanamke halafu huutaki "u-girly" wake?Mwanamke in a very simple narration,is a big girl.
 
Matatizo madogo kama haya ndio ayatolee taarifa Kwa waziri?. Hapo mtaani kwao hakuna mjumbe, serikali ya mtaa hakuna?. Mambo madogo kama haya yadhughurikiwe na waziri?.
...Kwako hili ni Jambo dogo. na halina Hadhi ya Kumshughulisha Waziri ??? [emoji848][emoji848]
hao Serikali ya mtaa SI WALIPASWA kuliona ??
 
Anzia serikali ya mtaani kwako na acha umbea kuingilia nyumba za watu. Muache aendelee kumtesa au uchukue huyo mtoto uishi nae kwako umlee vile unavyoona wewe inafaa.

Watoto wa mitaani watapngezeka Kwa serikali hii ya ccm.
Point ni moja tu hapo kuanzia serikali ya Mtaa ila vingine umeongeao nonsense kabisa
Otherwise huna mtoto ndo maana unaongea utumbo kama huu
 
Lakini,yeye ni mwanamke halafu huutaki "u-girly" wake?Mwanamke in a very simple narration,is a big girl.
Hapo anapokuwa too girly ndio watu wanamchukulia poa.

Ndio kama bungeni alipokuwa anaongelea mmomonyoko wa maadili kha ndio alijize vile, ata wanawake wenzake ambao awafikii akili zake hawana madoide yake (but that’s her personality) too girly.

Ukiachana na Dorothy ambae kichwa, ukiwauliza watanzania nani mwamamke kichwa bungeni not many can tell you Ndalichako ndio mwenye degree ngumu (kati ya wabunge wa jinsia zote) nonetheless she is a very bad politician na ukimsikiliza uoni dalili za uwezo wake. Tofauti na Dorothy even spontaneously kwenye vichambo vyake she is academic.

Dorothy Gwajima ni genius

Good morning šŸ‘‹
 
Sasa,hebu turudi "Rau madukani"!Tujiulize.Huyo mtoto ni wa nani?Ametokea wapi?Kwa nini aajiriwe uyaya kwa umri huo?Hapo awali aliishije?Wapi na wapi?Halafu turudi sasa kwa mama Nancy.Kwa nini amemchukua awe yaya wake?Ni yaya kweli?Ni ndugu in yayas disguise?Hitimisho;Mama Nancy atamalizana na serikali "kiungwana".Vipi muendelezo wa mtoto/"yaya" kimaisha yake?
duuuh,,apo kingine tunaweza sema tumtoe pale yule mtoto kumbe mazingira aliyotoka ndo magumu zaidi ya hayo kwa mama Nancy,coz miaka 10 ni mdogo sana jamani,lazima kuna mengi nyuma ya pazia,,sawa atatolewa pale je anaweza pata msaada wa kudumu !?
 
Back
Top Bottom