mtoto wa miezi nane anasumbuliwa na malaria mara kwa mara..

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2008
Posts
281
Reaction score
66
wadau nahitaji msaada wenu, naamini wengi hapa wanafamilia au wanaufaham ufaham kuhusu mambo ya watoto.
Kuna mtoto wa mdogo wangu anaugua mara kwa mara. Mara ya kwanza mtoto alikua anatapika kila akipewa chakula.
kwenda dispensary ya karibu wakampima wakasema ana malaria. wakampa dawa na kumchoma sindano kuzuia kutapika.
hali ikatulia kidgo lakini baada ya kama wiki 2 tena ile hali ikajirudia. kwa sasa ni zaidi ya mara 3 ipo hivyo na wanamwambia ana malaria 2. kabadilishiwa dawa lakini wapi. Kaniomba ushauri nikasema ngoja niulizie kwa watu. Hivyo wadau naomba kuuliza maswali yafuatayo:

1) Ni hospital/Dispensary gani ambayo ni affordable lakini wanahuduma nzuri sana kwa uzoefu wako hasa mambo yanayosumbua watoto?

2) Kuna Dr yeyote wa watoto unayemfaham au hospital/Dispensary yake ambayo sio ghali sana anaweza kumpeleka huyu mtoto akachekiwe.

Ni hayo tu kwani nimeona inaweza kuwa tatizo ni zaidi ya hayo malaria 2 wanayomwambia kila akienda kwenye dispensary ya hapo mtaani kwako.

Natanguliza shukrani
 

hiyo isiyo ghari sana unaongelea about kiac gan ghar kwako kwa mwingine inakua kawaida tu
 
ahsante mkuu concious mind, kusema kiasi inakuwa ngumu kwani mara nyingi itategemea na tatizo, lakini kwa wazoefu nafikiri wanaweza kujua hospital nafuu kwa ujumla wake. Inaweza kuwa 70,000 au chini ya hapo.
 
Kama upo Temeke mpeleke kwa Dr. Massawe, yupo jirani na Temeke Hospital.
 
Kazi si kuzaa kutia mimba, kazi kulea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…