Mtoto wa mwaka na nusu hatembei

Mtoto wa mwaka na nusu hatembei

Kifaranga

Senior Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
144
Reaction score
31
Wakuu habari za muda huu, nina rafiki angu ambaye ana mtoto wa kike ambaye sasa hivi anatimiza mwaka na miezi 7 hivi takribani sasa mpaka leo huyo mtoto hajatembea kabisa shida itakuwa ni nini alienda Muhimbili wakamuambia hilo tatizo halitibiki chakufanya waendelee kumfanyisha mazoezi.

Je kuna mwenye utaalam zaidi wa kushauri?

Asanteni.
 
Wakuu habari za muda huu, nina rafiki angu ambaye ana mtoto wa kike ambaye sasa hivi anatimiza mwaka na miezi 7 hv takriban. Sasa mpaka leo huyo mtoto hajatembea kabisa. Shida itakuwa ni nini?

Alienda Muhimbili wakamuambia hilo tatizo halitibiki chakufanya waendelee kumfanyisha mazoezi.

Je kuna mwenye utaalam zaidi wa kushauri?

Asanteni.
siyo tatizo labda kama ana viashiria ambavyo siyo vizuri. Binti yangu alitembea na mwaka mmoja na miezi kama tisa hivi, alikuwa anawacheka sana wadogo zake wa miezi nane wanaotembea na yeye hata kuendesha gari la miguu mitatu alikuwa analiogopa, ni changamoto sana, unaweza pia kumwona daktari kama una wasiwasi sana.
 
Vitu vya kawaida unless muwe mume-notice kitu ambacho si cha kawaida. Kama anacheza, anasimamia vitu, vurugu kama kawa, hiyo ni kawaida!

Kama anaishi na baba yake, awe anamrusha rusha na kumpandisha kwenye vitu kama meza, stuli, viti na vinginevyo na kumuachilia hapo huku umemsimamia! Inaonekana ni muoga akisimama akiona height anahofu kuanguka! Tiba za kienyeji hizo 🤣🤣🤣🤣
 
Mtoto wangu alikuwa na shida kama hiyo..ni ukweli inatakiwa mazoei lakini mzazi pia unatakiwa kuwa serious sana ili kumsaidia mtoto kutembea.
Nilichofanya nilinunua michezo mingi sana yenye rangi tofauti ikawa inamvutia kuifuata..kisha nikawa namsaidia kumshika akiwa anatembea baadaye namwachia..mwanzo alikuwa akiogopa baadaye akazoea akaona kama sehemu ya mchezo huku nikawa na mwekea muziki anacheza Choir..
Nilifanya zoezi hili kwa mda miezi 4 baadaye akawa sawa..
Ushauri:
Jitahidi kumtembeza kwenye mchanga bila ya kuvaa viatu
Mzazi atumie mda mwingi kuwa na mtoto kwenye mazoezi
Mwongeze msosi hasa maziwa ya ng'ombe ya kienyeji anywe kila siku,dagaaa na matunda
Huwe unampeleka kwenye mazoezi ya viungo wanyoshe miguu.

Ukifanya hivyo naamini mtoto wako atatemebea ndani ya miezi 3
 
Kawaida mtoto anapofikisha wiki sita anatakiwa aonwe na daktari wa watoto kwa review. Hapa kuna mengi hubainika kama kuna tatizo.

Muons daktari wa watoto upate ushauri.
Oooh kumbe.nikizaa tena nitampeleka.wa kwangu ametembea Na miezi Tisa.siku hizi anakimbia tu.
 
Watakuwa walikuwa hawamfanyii mazoezi ya kutosha! Wazazi wa Dar bhana!!
 
kwa mujibu wa coments nyingi inaonesha huyo mwenye mtoto huenda akawa ndio wale wa maisha ya kizungu, mtoto mda wote anatembezwa kwenye kitoroli... mwambie huyo mzazi abadilike
 
Mbona kawaida sana hiyo, unless kuna something strange ume note, wangu pia alitembea akiwa na mwaka mmoja na miezi sita, wapo wanaofanyiwa makanjanja yani ndani ya miezi saba tu unapishana nako kwa sebule.
Kama mgeni unaweza toka nduki
 
Naomba unijibu haya maswali?
-Mama wakati anajifungua hakupata shida yoyote ya uzazi na mtoto alilia mapema au kunyonya mapema baada ya kuwa amezaliwa?
-Mtoto amekomaa shingo na kukaa akiwa na umri gani?
-Ameanza kutambaa?,kama anatambaa anatambaa kwa matako au miguu?
-Ana kilo ngapi sasa?
-Kwa jitihada za yeye kutembea ametafutiwa baby walker(kile kitoroli ambacho mtoto anaingia ndani ili atembee)?
 
Wakuu habari za muda huu, nina rafiki angu ambaye ana mtoto wa kike ambaye sasa hivi anatimiza mwaka na miezi 7 hv takriban. Sasa mpaka leo huyo mtoto hajatembea kabisa. Shida itakuwa ni nini?

Alienda Muhimbili wakamuambia hilo tatizo halitibiki chakufanya waendelee kumfanyisha mazoezi.

Je kuna mwenye utaalam zaidi wa kushauri?

Asanteni.
Hatembei kivipi?Anatambaa?Anasimama?Ananyanyua miguu kidogo akishikwa?Anaweza kutembea na ukuta?
 
H
Wakuu habari za muda huu, nina rafiki angu ambaye ana mtoto wa kike ambaye sasa hivi anatimiza mwaka na miezi 7 hivi takribani sasa mpaka leo huyo mtoto hajatembea kabisa shida itakuwa ni nini alienda Muhimbili wakamuambia hilo tatizo halitibiki chakufanya waendelee kumfanyisha mazoezi.

Je kuna mwenye utaalam zaidi wa kushauri?

Asanteni.
Huwenda sio tatizo mi bint yangu alitembea na miaka 2
 
siyo tatizo labda kama ana viashiria ambavyo siyo vizuri. Binti yangu alitembea na mwaka mmoja na miezi kama tisa hivi, alikuwa anawacheka sana wadogo zake wa miezi nane wanaotembea na yeye hata kuendesha gari la miguu mitatu alikuwa analiogopa, ni changamoto sana, unaweza pia kumwona daktari kama una wasiwasi sana.
Shida ipo kwamba mpaka sasa hivi hajaweza kukaa mpaka kusimama, walienda CCBRT wao wanamuambia tu mazoezi kwa wingi
 
Fika hospital kwanza mkuu kwa wataalamu wamcheki mtoto ili kama kuna tatizo liahiwe mapema kabla halijawa chronic.

All the best
Asante mkuu, alienda Muhimbili ndio wakamuambia tatizo lake halitibiki sanasana mazoezi, kabla ya hapo alishaenda CCBRT wanamchke kisha wanampa tarehe nyingine ya kwenda
 
Back
Top Bottom