Mtoto wa mwaka na nusu hatembei

Mtoto wa mwaka na nusu hatembei

Naomba unijibu haya maswali?
-Mama wakati anajifungua hakupata shida yoyote ya uzazi na mtoto alilia mapema au kunyonya mapema baada ya kuwa amezaliwa? Hakupata shida yeyote, mtoto alilia vizuri tu na alinyonya maziwa ya mama yake punde tu
-Mtoto amekomaa shingo na kukaa akiwa na umri gani? kwa mujibu wa jamaa ananiambia bado hajaweza kusimama wala kukaaa,
-Ameanza kutambaa?,kama anatambaa anatambaa kwa matako au miguu? nafikriri hata kutambaaa bado kama hajaweza kusimama wala kukaa.
-Ana kilo ngapi sasa? Roughly kilo kama 8 hivi
-Kwa jitihada za yeye kutembea ametafutiwa baby walker(kile kitoroli ambacho mtoto anaingia ndani ili atembee)? ana kibaiskeli sema ndo hvyo shida hawezi kukitumia
 
Wakuu habari za muda huu, nina rafiki angu ambaye ana mtoto wa kike ambaye sasa hivi anatimiza mwaka na miezi 7 hivi takribani sasa mpaka leo huyo mtoto hajatembea kabisa shida itakuwa ni nini alienda Muhimbili wakamuambia hilo tatizo halitibiki chakufanya waendelee kumfanyisha mazoezi.

Je kuna mwenye utaalam zaidi wa kushauri?

Asanteni.
Pia jamaa ananiambia kipindi cha nyuma alishawahi kuugua ugonjwa wa Manjano nadhani ndio imeleta shida zote hizi.
 
kwa mujibu wa coments nyingi inaonesha huyo mwenye mtoto huenda akawa ndio wale wa maisha ya kizungu, mtoto mda wote anatembezwa kwenye kitoroli... mwambie huyo mzazi abadilike
Hapana huyu ni wa hali ya chini kabisaa kabisaa ni maskini kabisa, baba yake ana vibarua vya hapa na pale tu vya kumuingizia kipato, yaani hayupo kwenye ajira rasmi.
 
Wa kwangu ana miaka na miezi miwili anasimama ila hatembeii je ni tatizoo?
 
Back
Top Bottom