Mtoto wa My Girlfriend wangu hajatulia

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
16,717
Reaction score
13,176
Habari zenu za usiku huu wanajamvi,
Ni hivi mimi nina My girlfriend wangu ambaye teyari ana mtoto na jamaa mwengine,ila huyu mtoto wake hajatulia kwa kweli na huyu mama yake simuoni kuchukua hatua zozote kuhusu hilo anamdekeza sana bana mie inaniuma lakini nikumuambia anasema mie silipendi kinda lake hilo,
Siku moja nilikwenda na rafiki yangu kumtembelea yaani ilikuwa ni aibu mara kamsachi huyo rafiki yangu,mara kutoka nje kaanza kurusha mawe ndani,mara kachukua chupa ya konyagi tuliyokuwa tunakunywa na kupiga fundo moja,yaani ni maudhi kwa kweli kwenda kumtembelea na hata anapotaka kuja kunitembelea akiniambia anakuja na hilo kinda lake binafsi nakosa raha najua lazima atanitia aibu/hasara ya kuvunja vitu,
Kuna cku uzalendo ulinishinda nikamuambia kuwa huyu mtoto wako kwa kweli mie siikubali tabia yake yaani umemlea kama yai unaogopa lisipasuke,basi adhabu niliyopewa ni kunyimwa uroda miezi mitatu.
Naomba ushauri wenu wana jamvi nimfanyeje mama yake ili amrekebishe huyu mtoto wake?
 
Ushapenda tena, vumilia tu!
 
Ujanja wote huo mtoto wa kwanza umeanziwa na mwenzio. Nunua mpya achana na "second hand" zinasumbua sana.
 
Ujanja wote huo mtoto wa kwanza umeanziwa na mwenzio. Nunua mpya achana na "second hand" zinasumbua sana.
hahahahahaaa hii ni nyumba ndogo yangu sio my wife wangu wa kunyumba
 
Ukipenda boga penda na ua lake.

Komaa broda acha kuzenguliwa na watu eti used. Used ndo bomba sana
Magari yeliyotumika ndo mchicha kinoma yaani huna haja kuhangaika na oil mule mule bro
 
Ushapenda tena, vumilia tu!
kuvumilia mkuu mbona naona kazi itakuwepo maana mimi ni mtu wa ghadhabu ipo cku nitampa kipigo cha mbwa mwizi halafu tutamaindiana bure na huyu mama yake
 
Ukipenda boga penda na ua lake.

Komaa broda acha kuzenguliwa na watu eti used. Used ndo bomba sana
Magari yeliyotumika ndo mchicha kinoma yaani huna haja kuhangaika na oil mule mule bro
yaani niendelee kumvumilia kwa style hii,yaani unaweza kusema ni mtoto wa kuchakachuliwa maana dah!anasumbua kwa kweli
 
roho mbaya tu,angekuwa wako ungeandika uloandika hapa:embarassed2:
 
hahahahahaaa hii ni nyumba ndogo yangu sio my wife wangu wa kunyumba

sasa kama nyumba ndogo mambo mengine unapotezea.
Pata utamu, ya familia yake yaache.
Kuna mdau alisema humu kuwa hutakiwa kuwa na wivu na mpango wa kando.
 
roho mbaya tu,angekuwa wako ungeandika uloandika hapa:embarassed2:
roho mbaya ipi?binafsi ninayo makinda matatu lakini hakuna hata mmoja mwenye tabia kama ya huyu mie nawapeleka kijeshi
 
sasa kama nyumba ndogo mambo mengine unapotezea.
Pata utamu, ya familia yake yaache.
Kuna mdau alisema humu kuwa hutakiwa kuwa na wivu na mpango wa kando.
nashukuru kwa ushauri nitaachana naye ili amlee hivyo hivyo kama yai
 
Mkuu
Pole sana.
Mapenzi yanatakiwa yawe pande zote mbili, ila naona kunadalili za mapenzi ya wewe tu kumpenda huyo mdada
Isitoshe inaonekana huyo mdada sio msikivu, na ana dalili zote za kukudharau.
Nahisi pia huyo jamaa aliyemzalisha bado anapendwa na huyo mdada kiasi cha kwamba usije kushangaa ukakuta wanatoka gesti wameshikana viuno au amekuletea mimba ya nje akadai ya kwako.
Chukua hatua kabla ya hatari,
Kama mpo kwa ajiri ya play games na una muda wa kufanya nae hivyo sawa, lakin hafai kabisa kuwa mkeo
 
roho mbaya ipi?binafsi ninayo makinda matatu lakini hakuna hata mmoja mwenye tabia kama ya huyu mie nawapeleka kijeshi

kwa kuwa huna wa kukuambia kuhusu tabia za wanao,hayakuhusu ana babake huyo fanya kilichokupeleka.
 
Binafsi sina future naye ni kuchakachuana tu basi ila natumia salama kaka sichezi pekupeku naogopa uwanja wenyewe una mbigili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…