Mtoto wa Zidane, Enzo astaafu soka akiwa na Umri wa miaka 29

Mtoto wa Zidane, Enzo astaafu soka akiwa na Umri wa miaka 29

Kidogo Marcus Thuram anajitahidi huyu mtoto wa Lilian Thuram. Lakini pia nimeona mtoto wa Patrick Kluivert anaitwa Justin Kluivert naye anajitahidi. Ila hawa watoto wa Beckam na Maldini naona wanaenda kama wa Zidane japo walau wa Zidane kakomaa mpaka miaka 28.

Sio wakati wote maji yatafuata mkondo
 
Alfie Halaand =
Erling Halaand.
Peter Schmeichel=
Kasper Schmeichel.
Cesare Maldini =
Paolo Maldini
Johan Cruyff=
Jordi Cruyff
Paolo Maldini =
Daniel Maldini.
Harry Redknapp=
Jamie Redknapp
Orodha hii pia ni ndefu sana
Mkuu ,kuna tofauti kati ya kucheza mpira na kucheza mpira Kwa umahiri
Hao kweli ni watoto wa wachezaji nyota ila wao wenyewe sio nyota kabisa ukimuondoa Erling Haaland na Maldini's family
Wengine ni average players. Mm nimeuliza wachezaji ambao ni nyota kama ilivyokua babaake
Good observation,anyways.
 
Hivi kuna mwanasoka gani mahiri ambae mtoto wake nae alikua mchezaji mahiri?
Pele
Maradona
Garincha
Frank Rjikaard
Kluivert
Beckham
Ronaldo
Figo
Zidane
Ronaldinho
List ni ndefu
Naona Marcus Thuram anapambana pale Inter Milan. Huyu ni mtoto wa mchezaji Lilian Thuram. Wale walioshuhudia kombe la dunia la mwaka 1998 watakuwa wanamkumbuka. Kumbe na mimi nazeeka sasa!
 
Enzo Zidane, mtoto wa Zinedine Zidane, ameamua kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 29. Enzo aliwahi kuchezea klabu ya Real Madrid na vilabu vingine, lakini sasa ameamua kustaafu soka.

Enzo Zidane alianza safari yake ya soka akiwa bado kijana mdogo, akifuata nyayo za baba yake Zinedine Zidane. Enzo alijiunga na academy ya Real Madrid, maarufu kama "La Fabrica", ambapo alifanikiwa kuonesha kipaji chake na kujitengenezea jina lake mwenyewe. Ingawa alikabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na ukubwa wa jina la familia yake (Zidane), Enzo aliweza kuonyesha uwezo wake uwanjani.

Baada ya muda akiwa kwenye academy ya Real Madrid, Enzo alipandishwa hadi timu ya wakubwa ya Real Madrid, lakini nafasi yake ya kucheza katika kikosi hicho ilikuwa finyu kutokana na ushindani mkali ndani ya timu hiyo. Hii ilimfanya Enzo kutafuta fursa za kucheza katika vilabu vingine, aliamua kutimkia klabu Deportivo Alavés kwa mkopo. Huko, alijaribu kupata muda na nafasi ya kucheza zaidi na kuonyesha uwezo wake.

Safari ya Enzo haikuwa rahisi, kwani alihamia vilabu kadhaa tofauti katika juhudi za kupata nafasi ya kudumu ya kuonyesha kipaji chake. Alicheza kwenye vilabu vya Lausanne-Sport ya nchini Uswisi, Desportivo das Aves ya nchini Ureno, na Almería ya nchini Hispania. Ingawa alionyesha uwezo wake katika vilabu hivi, hakupata nafasi ya kudumu kama alivyotarajia.

Uamuzi wa Enzo kustaafu soka umekuja baada ya kutafakari kwa kina kuhusu mustakabali wake. Katika taarifa aliyotoa, Enzo ameeleza kuwa amefurahia safari yake ya soka na anashukuru kwa fursa alizopata, lakini kwa sasa anahisi ni wakati wa kuanza changamoto mpya katika maisha yake. Aliongeza kuwa anapanga kuendelea kuwa karibu na soka,na kujaribu fursa zingine kama ukocha.
View attachment 3106111
Arnde akale pizza tu, soka siyo mchezo wa vijana watokao familia zenye hela. Wanaocheza soka ambao hutoka familia zenye hela wengi huenda kucheza soka ili wapate jasho la kuogea tu au baba zao hukaribu kuendeleza ndoto na mapenzi yao kupiyia watoto wao lakini watoto wakikua na kujitambua hujiamulia ya kwao.
 
Hivi kuna mwanasoka gani mahiri ambae mtoto wake nae alikua mchezaji mahiri?
Pele
Maradona
Garincha
Frank Rjikaard
Kluivert
Beckham
Ronaldo
Figo
Zidane
Ronaldinho
List ni ndefu
Labda Afrika, Ulaya na America ni wa kuhesabu
 
Mkuu ,kuna tofauti kati ya kucheza mpira na kucheza mpira Kwa umahiri
Hao kweli ni watoto wa wachezaji nyota ila wao wenyewe sio nyota kabisa ukimuondoa Erling Haaland na Maldini's family
Wengine ni average players. Mm nimeuliza wachezaji ambao ni nyota kama ilivyokua babaake
Good observation,anyways.
Haiwezekani kufanana kila kitu.
Kuna baadhi ya familia baba alikuwa na uwezo mkubwa kuliko mtoto lakini kuna ambao baba alikuwa mchezaji wa kawaida kuliko mwana.
Wachache kati yao walitikisa baba na mtoto.
Tunachoangalia wote wamechezea timu za madaraja ya juu na wengine kwenye timu za mataifa yao.
 
Wapo wakina mao mkami na kijana wake Himid Mao

Wapo wakina Sure boy

Wapo wakina Ngasa

Wapo wakina Maftaa

Wapo wakina Manyika

Wapo wakina tegete

Huku kwetu kiasi chake tumeweza...


Huko Ulaya ni wachache sana kama wakina Jini la Man city...
Wachezaji wachangani hao njaa tu ila hawana kipaji chochote... kibongobongo mwenye kipaji Samata tu aliyevuka abroad
 
images-2.jpeg
 
Naona Marcus Thuram anapambana pale Inter Milan. Huyu ni mtoto wa mchezaji Lilian Thuram. Wale walioshuhudia kombe la dunia la mwaka 1998 watakuwa wanamkumbuka. Kumbe na mimi nazeeka sasa!
Labda atafuata nyayo za babaake
 
Hivi kuna mwanasoka gani mahiri ambae mtoto wake nae alikua mchezaji mahiri?
Pele
Maradona
Garincha
Frank Rjikaard
Kluivert
Beckham
Ronaldo
Figo
Zidane
Ronaldinho
List ni ndefu
Lilian Thuram mwanae anaitwa Marcus Thuram anakipiga pale Inter Milan Italy Tena ni first eleven Kuna kipindi anamuweka bench Lautaro Martinez nyota kutoka Argentina. Pia Kuna Timothy Weah mtoto wa nyota wa zamani wa AC Milan na Rais wa Liberia. Timothy Weah anacheza timu ya taifa ya Marekani first eleven.
 
Back
Top Bottom