Mtoto wangu ana shida ya ngozi

Spear_

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Posts
1,615
Reaction score
545
Mtoto wangu ana shida ya Ngozi...anatokewa na vipele vinamwasha sana...ngozi inakauka na kukakamaa alianzwa akiwa na wiki 2 tukafikiri ni vipele vya joto lakini

vimeendelea mpaka sasa ana miezi 6 kwa kwel ni mateso kwa mtoto tumeshaenda kwa wataalam wa Ngozi mpk KCMC mwanzo wakasema ni Eczema wakampa dawa alipotumia vipele na mwasho viliisha but dawa ilipoisha vikarudi tena tukarudi wakatubadilishia dawa but ikawa the same mwenye uelewa wa dawa ya huu ugonjwa pls mtoto mchana halali kabisa ni kujikuna tu....

Asante
 
ni sawa walivyokuambia inaitwa pumu ya ngozi. mi wakwangu alikuwa na hilo tatizo nilimpeleka kwa dr wa kihindi kariakoo jina limenitoka, kuna dawa alimpatia jina nimelisahau kwa sababu miaka mitatu imepita haikuchukua wiki mbili tatizo likaisha ingawa pia nilitumia mafuta ya ubuyu kipindi kile yanavuma ingawa niliyaacha mapema baada ya watu kututisha kuhusu hayo mafuta ingawa naamini kati ya dawa au mafuta kimoja kilimsaidia.Sasa ana miaka minne hana hata shida nae pia alizaliwa na hilo tatizo, wengine wanasema kadri atakavyokuwa tatizo litaisha,
 
Asante kwa kunitia moyo....ninaamini na wa kwangu atapona
 
Mafuta ya ubuyu ulikuwa unampka? au ulikuwa unayatumiaje?
 
Mpake dawa ya vidonda inaitwa Iodine. Kama ni mba au fungus watakwisha...
 
Mafuta ya ubuyu ulikuwa unampka? au ulikuwa unayatumiaje?
Mkuu ningekushauri usimpake mafuta ya ubuyu bila kupata maelekezo watoto wanatofautiana...mi wa kwangu tumezoea tunampaka olive oil kwa bahati mbaya juzi nilichanganya chupa nikampaka hayo ya ubuyu( vichupa vinafanana) yani aliota vipere habari...nakushauri ungeuliza kwanza..
 
mnamuogeshea sabuni gani na kumpaka mafuta gani?
 
asante kwa ushauri
 
mnamuogeshea sabuni gani na kumpaka mafuta gani?

tunamwogeshea sabuni ya kipande nafikiri ni jamaa....mafuta anatumia Vaseline Seal Blue isiyo na harufu...pia tunampka Zincast Baby Cream kumpunguzia mwasho
 
Mnaweza kumjaribu, sabuni ya kipande inaitwa mbuni na mafuta ya Nazi ya kutengeneza mwenyewe nyumbani(sio ya kununua dukani,mengi hayaaminiki) alafu mumsikilizie
 
Mnaweza kumjaribu, sabuni ya kipande inaitwa mbuni na mafuta ya Nazi ya kutengeneza mwenyewe nyumbani(sio ya kununua dukani,mengi hayaaminiki) alafu mumsikilizie
asante
 
tunamwogeshea sabuni ya kipande nafikiri ni jamaa....mafuta anatumia Vaseline Seal Blue isiyo na harufu...pia tunampka Zincast Baby Cream kumpunguzia mwasho
jamaa sio multipurpose kama kuku,komoa and the like, jamaa PH yake kubwa sanaa ni kwa kutolea uchafu nguo tu na vyombo labda
 
Mkuu kama uko Dar nakushauri umpeleke cannosa hisp. kwa masister ipo tegeta wakwangu alikuwa na tatizo hilo lakini walinipa dawa na tatizo limeisha hata kabla sijamaliza doze.
 
Mkuu kama uko Dar nakushauri umpeleke cannosa hisp. kwa masister ipo tegeta wakwangu alikuwa na tatizo hilo lakini walinipa dawa na tatizo limeisha hata kabla sijamaliza doze.
niko Arusha mkuu,
 
jamaa sio multipurpose kama kuku,komoa and the like, jamaa PH yake kubwa sanaa ni kwa kutolea uchafu nguo tu na vyombo labda

mkuu unashauri tutumie sabuni ya kuku au komoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…