Mtoto wangu analilia sana.Naomba ushauri.

mwankuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2010
Posts
334
Reaction score
120
Poleni na majukumu wakuu.

Nina mtoto (kike) ana miaka miwili.Tangu azaliwe amekuwa akililia sana.Wakati anazaliwa ilionekana ni kawaida lakini kadri muda unavyoenda ndivyo anavyozidi kulilia bila hata sababu.

Nafikiria pengine ana matatizo fulani au hata tabia ya kulilia inaweza ikawa na madhara kiafya.Nimewahi kwenda hospitali lakini nikaambiwa hakuna tatizo ni hali ya kawaida.Kuna wakati hatulali usiku kwa sababu ya kulilia motto.

Kama unajua au una experience na haya mambo naomba mdaada
 

Unasema analia bila sababu? Si kweli inasemwa kati ya viumbe wasio na unafdiki na uongo basi ni watoto! Akifurahi atacheka na akikerwa na kitu atalia tu! Mwanao anakupa ujumbe kuwa kuna kitu kinamsumbua usichukulie ni kitu kidogo hicho. Mwanao kuna kitu kinamtesa acha yote ushughulikie afya ya mwanao. Mwone specialist wa watoto usichoke ndugu yangu! Hangaika umtoe kwenye mateso mwanao..akikosa raha nawe utakosa amani muda mwingi.fanya hivyo.pole sana
 

Mkuu umefikisha ujumbe katika style ambayo inagusa sana. Kwa ujumla umetoa ushauri mzuri, "thumb up"
 
Inawezekana mtoto hashibi chakula? Hebu mpe diet ya milo 5 kwa siku uone itakuwaje.
 
Watoto wa siku hizi wana njaa sana, feed the child please.
 
umejuaje analia sana?umewahi kuwa na mtoto mwingine?
 

Mkuu fanya umuone Dk Masawe yupo pale Moroko pembeni ya makao makuu ya Airtel,yule jamaa ni kiboko wa magonjwa ya watoto.Ila kupata appointment pale inabidi uwahi saa 6 usiku uwe pale na mnakesha mpaka asubuhi saa 2 kuwahi namba,anahudumia wagonjwa kumi tu kwa siku.
 

Nakushauri umpeleke kwa watumishi wa mungu akaombewe kwani huwezi jua labda vitu vibaya vinamsumbua
 
Wengine wanatabia ya asili ya kisirani,
pengine ana maumivu sehemu fulani ya mwili wake,
pengine mnampatia chakula kidogo mno,
pengine haujakamilisha taratibu za wazee,
makisio ni mengi,
 
"analilia" neno ulilotumia limezua utata kidogo, binafsi sijakuelewa. maana swali la kwanza, analilia nini?
 
Huyu kadata alimaanisha kulialia na si kulilia
 
Ndugu hata mm Hyao yalinitokea kwa Mwanangu, kiukweli Hapo unapokaa sio pazuri,hiyo nyumba au hapo mtaani kuna vitu vinamtesa mwanao, ni mambo ya kichawi amini usiamini. Ushauri wangu kwako, kama ni mkristo mpeleke kanisani akaombewe, na kama muislam tafuta shehe amsomee,au tafuta Mtaalam. haya mambo yapo.pole sana.
 

mpatie chakula ashibe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…